Mchezaji wa timu ya Yanga Juma Abdul akijaribu kunyang'anya mpira kutoka kwa beki wa timu ya Atletico Henry Mbazumutima kwenye  mchezo wa pili wa fungua dimba katika michuano ya kombe la Kagame inayoandaliwa na shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA inayofanyika jijini Dar es salaam Tanzania, Mpira umekiwasha na timu ya Yanga imeambulia kipigo cha magoli 2-0 yaliyofungwa na mchezji Didier Kavumbagu wa Atletico. Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2012

    Hivi huyu kocha wa Yanga si alisema anakuja kufanya maajabu hapa Tanzania? Ngoja sasa aone mpira wa Bongo ulivyo, atakimbia mwenyewe na mshahara ataacha. Hapa hakuna mpira ni uchawi tu, na ndiyo maana hakuna talent na wachezaji hawafundishiki. Pole mzungu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2012

    Mimi huwa nashangaa sana watu wanaposema Tanzania kina vipaji vya soka. Yanga ni timu ya miaka kibao, na tena siku zote inacheza katika nchi yenye amani, haya hivyo vipaji si ndio tungeviona sasa. Viko wapi? Ujinga mtupu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2012

    Huyo kocha ana mdomo sana,huwezi kutegemea makubwa mara moja.Halafu anashangaza ana linganisha mpira wa Yanga na wa Arsenal ,Barcelona na Real Madrid.Aache majigambo afundishe mpira.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2012

    FA TZ INAFANYA JITIHADA GANI KUHAKIKISHA WASHABIKI WANAFIKA UWANJANI KUJIONEA MASHINDANO HAYA.

    NI AIBU TIMU KUBWA TANZANIA, YANGA INACHEZA DAR HUKU UWANJA UKIWA MTUPU KABISAAAA.

    KUNA FAIDA GANI KUWEKA KIINGILIO KIKUBWA NA KUPATA WATAZAMAJI WACHACHE WAKATI WINGI WA WATAZAMAJI HUSAIDIA KUHAMASIHA TIMU ZA NYUMBANI.

    FA AU FAT KAMA ILIVYOKUWA IKIJULIKANA HUKO NYUMA, ILIANGALIE SUALA HILI.

    NATUMAI KAMATI YA MASHINDANO YA CECAFA KWA KUSHIKIRIANA NA FA TZ WATALIONA HILI NA KULIFANYIA KAZI HARAKA.

    NEXT MATCHES TIMU YA NYUMBANI IKICHEZA, UWANJA UJAE!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...