LEKA DUTIGITE KIGOMA.. ni tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika mkoani Kigoma tarehe 17 ndani ya mwezi huu wa saba na kuwashwa moto na wasanii wazawa wa kigoma. Mpaka sasa ari waliyonayo wasanii hao ni ya kubwa mno.. mpaka imekuwa kama ni changamoto kwa wasanii wanaotoka katika mikoa mingine, na kulowea zaidi Dar es Salaam. Hata hivyo breaking news inaonyesha kuwa karibia nusu ya nyimbo zinazofanya vizuri hivi sasa katika soko la muziki hapa nchini ni za wasanii wanaotoka katika mkoa wa kigoma. Angalia nyimbo kama "Kichwa kinauma" yake Ali Kiba aliyomshirikisha Jaydee, "Upepo" Recho, "Mawazo" Diamond, "Maneno maneno" Queen Darleen, "Jua ni wewe" Mwasiti akimshirikisha Ally Nipishe, Na nyingine nyingi kutoka kwa wasanii wao kina Chege, Abdu Kiba, Baba Levo, Makomandoo Bongo, Linex, Banana Zorro na wengine wengi.
Jambo lingine la kutia hamasa ni jinsi Mbunge wao wa Kigoma Zitto Kabwe anavyoshirikiana nao katika kila jambo. Naye msimamizi wa ama mratibu wa tamasha hilo Mwasiti Almas naye alifunguka na kusema haya "Kila kitu kwetu kama wasanii wa Kigoma kiko tayari kwa ajili ya tamasha hili, Kilichobaki ni wasanii wenyewe kufika mkoani kwao na kutimiza lengo la Tamasha hili, kwani tamasha hili linasimama kuwatia chachu ama hamasa vijana wa mkoa wa Kigoma mkoani humo".
keeep it up zitto...
ReplyDeleteZITTO ANAKUNYWA POMBE MUISLAMU WA NGUVU HAYA WATU WA KIGOMA
ReplyDeleteZitto naye anavaa saa ya dhababu, nini?
ReplyDeleteHata kama niko USA kwa sasa wala sijakulia Kigoma ila mimi ni "muha" kwa kabila, manyovu Kasulu ndiko waliko babu zangu. Nimefurahishwa sana na hii kitu, tuendelee kusupport tulikotoka ukizingatia Kgm ni mkoa uliosahaulika kidogo na wasanii wa sehemu zingine wachukue hii as a challenge. Here we go Kigomans. ONE ORIGIN, ONE LOVE, ONE NATION.
ReplyDeleteChezeya Ruge, wasanii , hamna pa kukimbilia, Mkipigia debe CHadema Ruge yupo,Mkipigia CCM RUge yupo, kazi kwenu!
ReplyDeleteHAYA BAHARIA KHAMSIN UMEWACHOKOZA WENZIO SASA UTAWABEBEA MBELEKO GANI MBINU ZA MIKOA
ReplyDeleteMdau wa Sat Jul 14, 08:47:00 PM 2012, acha ushamba. Hiyo sio pombe. Ni juice ya Apple, acha kujaji a book from its cover.
ReplyDeletemsimsahau mzee Bichuka wa Sikinde, Zahoro bangwe na wengine wengi pia wanatoka kigoma
ReplyDeleteila wengine wenu hapo mnatoka kigoma ya upande wa pili nna maana ya rwanda na burundi
Juice ya apple haina povu,I would not care less about what the guys drinks, hata kama anakunywa "kinibu", hayo ni maamuzi yake.
ReplyDeleteMdau kunywa Malta apple uone povu lake hata la safari cha mtoto kama kitu hujui funga mdomo. unaokena wewe ni mrugaruga.
ReplyDeletehuyo bwanawa kwanza issue iyoko hapa ni ya watoto wa kigoma, yeye analeta bombe na uislaam, uislam umekaza pombe kwa kuwa waislam wapo wanaokunjwa. nakuambia mtakoma kwa mfumo.
ReplyDelete