Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Megatrade, Gudluck Kway, akimkabidhi Katibu wa TASWA Arusha , Mussa juma, hundi ya sh 1.5 milioni, kama udhamini wa Kampuni hiyo katika bonanza la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, ambalo litafanyika julai 15 mwaka huu, makabidhiano hayo, yalifanyika palace Hoteli mjini Arusha.

Woinde Shizza,Arusha.

MAKAMPUNI kadhaa, yamejitokeza kudhamini Tamasha la saba la vyombo vya habari kanda ya Kaskazini, ambalo litafanyika Julai 15 katika Viwanja vya General Tyre mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Palace Hoteli, Katibu wa Chama cha waandishi wa habari za michezo na Burudani mkoa wa Arusha(TASWA ARUSHA), Mussa Juma alisema Makampuni ambayo yamekamilisha udhamini wake ni, Kampuni ya Bia nchini(TBL), Kampuni ya simu la Alphatel na Kampuni ya Megatrade Investment(T) Ltd.

Juma alisema wadhamini wengine ni Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA), Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na mengine kadhaa ambayo yatatangazwa hivi karibuni.

Katibu huyo, alisema katika tamasha la mwaka huu, zawadi mbali mbali zimetengwa kwa wanahabari, ikiwepo vikombe na fedha taslimu, katika kuhamasisha michezo na mahusiano baina ya wanahabari na taasisi nyingine Kanda ya Kaskazini.

Akizungumza wakati akikabidhi hundi ya sh.1.5,Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Megatrade Investment(T) Ltd, Godluck Kway, alisema kampuni hiyo, imeamua kudhamini bonanza hilo kama ishara ya kutambua jitihada za wanahabari mkoani Arusha.

Kway alisema kampuni hiyo, imejipanga kuhakikisha itachangia masuala ya kijamii, kutokana na sehemu ya faida ambayo wamekuwa wakipata kutokana na kuuza bidhaa zao mbali mbali za vinywaji vikali.

"hii ni mara yetu ya kwanza kusaidia tamasha hili, lakini tunaahidi tutaendelewa kufanya hivi katika miaka ijayo"alisema Kway.

Tamasha hili,ambalo hufanyika kila mwaka, huandaliwa na kampuni ya MS Unique Promotion kwa Kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za michezo(TASWA ARUSHA). na litahusisha michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia, kukimbiza kuku na kucheza muziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...