VOA Kiswahili inatafuta wazungumzaji kiswahili katika eneo la Tampa, Florida kushiriki katika matangazo yao ya mkutano mkuu wa uteuzi wa chama cha Republican wiki nzima hii. Kama upo Tampa na maeneo ya jirani mpigie simu Mwamoyo Hamza 202 441 9927. Shukran

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Madiaspora na Wabeba mabox mmneiona hii?

    Changamkeni muwasiliane na Dr.Hamza Mwamoyo ili mpate nafuu ya kazi ya Ukalimani wa Kiswahili angalau kwa muda kwa:

    1.Kushusha uzito mizigo migongoni kupunguza sugu za migongo na shingo kwa ubebaji wa mabox.

    2.Badala yake kuvaa mashati safi mkanda nje na tai (kiofisa) badala ya kushinda mkiwa mmevaa maovaroli na makoti ya mifuko na mikanda mingi ktk kazi ya UKULI!!!

    Ya nini tabu wakati ni mechi ya ushindi kabisa hii Refa akiwa Dr.Hamza Mwamoyo?

    ReplyDelete
  2. JAMANI WATU WALIOKOSA VISA NA WALIORUDISHWA BONGO NA UHAMIAJI WIVU WAO UMEKITHIRI KHA!

    ReplyDelete
  3. Mdau wa maoni Tue Aug 28, 02:44:00 PM 2012 nadhani hujaelewa wabeba box maana yake ni nini?
    Kwa kifupi ni wfanyakazi wa kitanzania ughaibuni na sio makuli kama unavyoeleza.
    Kuna madaktari ,mainjinia, wakandarasi,madereva(malori/delivery),wafanyakazi wa viwandani ,nk
    Kazi ni kazi la muhimu ni kupata rizki ya halali kwa familia yako na sio kama hayo unayosema .
    Kwani hapo bongo wafanyakazi wote wanapata rizki za halali?mbona rushwa kila kona ,dhulma, unyanyasaji makazini,ufisadi nk je haya ndio unayaona ya kuyavalia mkanda nje na tai shingoni?
    Ni maoni yangu tu

    ReplyDelete
  4. Wadau wa pili na wa tatu, ukiwa ugenini hata kama una PhD. yatakukuta kati ya haya hapa:

    (1.) Pamoja na Udakitari wako pana uwezekano utalipwa Mshahara kwa kiwango cha chini (under paid) kwa kuwa kila nchi inazingatia kuwapa kazi na maslahi makubwa Raia wake halisi na sio wewe (Raia wa kuandikishwa) uliyezaliwa na uliyetoka Tanzania.

    (2.) Pana uwezekano mkubwa pamoja na elimu yako ya Udakitari (kwa kuwa sio mwenyeji asilia) unaweza kupewa kazi ya kukata manyasi ya ng'ombe!

    YA NINI KUTUMIKA HUKO WAKATI HAMTHAMINIWI UGENINI?

    ACHENI UBISHI AJIRA YENU NA HESHIMA KWA KAZI YENU IPO NYUMBANI TANZANIA!

    ReplyDelete
  5. Hahahaha

    Mavazi ya kazi ngumu:

    Mdau wa kwanza, pana yale

    (1.)Makoti marefu yenye mifuko mifuko na mikanda mingi,

    (2.)Pana yale Ma Jeans yenye mikanda mabegani (BIG MARKS),

    (3.)Pana zile Over Rolls

    Maguo yote hayo matatu hapo juu yamekuwa yanatumika kwa kazi ngumu huku ktk wakati fulani Vijana wa Kisasa walikuwa wanatumia kuvaa kama Fashion hasa Mabaharia pamoja na kuvaa mabuti makubwaa!

    ReplyDelete
  6. Tatizo ugenini ni ugenini, si mchezo yaliyowakuta hawana ubishi wanaendelea huko Majuu kukaa kiubishi tu.

    ReplyDelete
  7. Enhee chezea Wazungu weye?

    Unaweza kusoma Darasa moja na Wazungu huko Majuu na ukawa anawaburuza kabisa kimasomo Darasani lakini engalia mkimaliza masomo utaona wenzio waleeee!.

    Wewe Maganga mwenye asili ya Tanzania hata kama umesomea Udakitari wa Binaadamu na ukapasi masomo vizuri zaidi wa wenzio Wazungu usije kushangaa ukakabidhiwa zizi la ng'ombe uwe Dakitari wa mifugo!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...