Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi UCF akichangia pesa kwenye harambee iliyoambatana na matembezi ya hisani kuanzia Buguruni hadi kwenye Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo ambapo zaidi ya Tsh129Millioni zilichangishwa.Pesa hizo ni kwaajili ya keneza kampeni yao ya dira ya mabadiliko mikoani kote kujiandaa na uchaguzi 2015.
 Prof.Lipumba akimuangalia Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Ilala Saidi Rico alipokua akichangia.
 Namna foleni ilivyokua wakati wa uchangiaji huo ambapo kila mmoja alipata fursa ya kusalimiana kwanza na Mwenyekiti huyo kisha ndio anachangia.
 Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba akiwa amembeba mmoja wa walemavu waliojitokeza kuchangia chama hicho kwenye viwanja vya Jangwani baada ya kumrukia na kumkumbatia.
Msongamano wa wanachama wa chama hicho kwenye foleni ya kwenda kuchangia fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. CUF muanze kuweka wagombea wepya kwenye nafasi ya Urais!!

    ReplyDelete
  2. Je hapa Nape Naue anasema je tena? Je na hawa wana mihela wanazopata nje ya nchi? Tutafurahi kusikia kauli ya CCM juu ya uchangaji fedha wa CUF kama walivyotoa kauli kwa CHADEMA.....

    ReplyDelete
  3. Ah! wanachama wa CUF wa miaka ile wameenda wapi? CUF kwishiney

    ReplyDelete
  4. Ruzuku inayotolewaga na serikali kwa chama hesabu zake ziko wapi mpaka mwatuchangisha?

    ReplyDelete
  5. MIgiro gombea URAISI utuondolee hii kelele ya Mie nataka uraisi Oh mie nataka uraisi! Hivi mlizaliwa kuwa maraisi? @#$%^&*(0

    ReplyDelete
  6. I like the sense of personal space in TZ queues!
    $D

    ReplyDelete
  7. Mbona naona hakuna kubagua kinamama na kinababa kuwa ktk foleni moja, kweli CUF imebadilika.
    Mdau
    Lumumba

    ReplyDelete
  8. Du huo mshikaki! sitaki kusema nakumbuka nikiwa kwenye basi la mbagala jamaa alinitunishia nafikiri kawea jiwe mfukoni kumbe ilikuwa tu ............!
    Kazi tunayo wabongo! Ustaaarabu yaani wasipobanana hivi hawafiki?

    ReplyDelete
  9. @ 04:26 PM

    Umenichekesha sana... hiyo inaitwa 'zero distance'

    ReplyDelete
  10. Foleni za kukaribiana namna hii ndio zinazaa MIFADHAIKO YA KISAIKOLOJIA na matokeo yake mnakuta mnaenda Kituo cha Polisi Posti cha karibu kuandikiana RB kwa kufungua Mashitaka badala ya kuendelea na zoezi la kuchangia Chama!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...