TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ALIUNDA KAMATI SIO TUME
Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa katika kikao chake na Waandishi wa Habari cha tarehe 4 Septemba, 2012, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alitoa taarifa ya kuunda Kamati  kuhusiana na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, tarehe 2 Septemba, 2012 ambapo katika vurugu hizo mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi alipoteza maisha.
Waziri Nchimbi alisema aliunda Kamati hiyo, (na siyo Tume), ili kumsaidia kupata majibu ya maswali yafuatayo, ambayo alisema hakuwa na majibu yake:
1.     Nini kilikuwa chanzo cha kifo cha mwandishi wa habari, Bw. Daudi Mwangosi,
2.     Kama upo uhasama kati ya waandishi wa habari wa Iringa na Polisi,
3.     Kama ipo orodha ya waandishi watatu (3) waliopangwa kushughulikiwa na Polisi,
4.     Kama ukubwa wa nguvu za Polisi zilizotumika ulikuwa sahihi,
5.     Kama zipo taratibu zinazoruhusu Vyama vya Siasa kukata rufaa visiporidhika na maamuzi ya Polisi,
6.     Kama kuna tatizo la mahusiano kati ya Polisi na Vyama vya Siasa.
Taarifa hii inatolewa ili kuweka sawa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tindu Lissu akisema Chama chake hakiungi mkono Tume ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha televisheni cha Channel Ten, kwa madai kwamba imeundwa kinyume cha Sheria ya Tume za Uchunguzi ya Mwaka 1962 Sura ya 29, ambayo alisema kwa mujibu wa Sheria hiyo, tume zote za uchunguzi huundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kupitia taarifa hii, tunapenda kuuarifu Umma kuwa Waziri Nchimbi hakuunda Tume ila aliunda Kamati hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kama Waziri na uundaji wa Kamati hii hauhusiani kwa vyovyote na matakwa ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Marejeo ya Mwaka 2002.
Utaratibu wa kutumia Kamati kutafiti jambo kwa kina kwa ajili ya kumshauri Waziri au kiongozi mwingine yoyote ni wa kawaida katika utendaji na utekelezaji wa majukumu ya umma.

Imetolewa na  Isaac J. Nantanga
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
06 Sepemba, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. We Tundu Lisu Mbayaaa we mbayaa kwa sheria, watu wame-copy na ku-paste umewaumbua mpaka wamebadili maneno yao wenyewe na kusema Waziri hakusema hivyo, kumbe amenukuliwa akisema hivyo hivyo kuwa anaunda Tume.

    ReplyDelete
  2. nini tofauti kati ya tume na kamati mi naona mizinguo tu hebu nifahamisheni nyie wenzangu mnaojua

    ReplyDelete
  3. Kweli Tundu Lissu na CHADEMA ni makini hawakurupuki.

    Ndiyo uzuri wa vyama vingi na kuwa na chama pinzani ambacho kina saidia serikali kujirekebisha pale ilipokosea.

    Mdau
    Mtazamaji

    ReplyDelete
  4. Hivi ni mimi tu naona tatizo hapa au kuna mwingine pia analiona? Kimsingi majibu ya maswali yote haya yanajulikana:

    1. Nini kilikuwa chanzo cha Kifo cha Mwangosi? -- Bomu
    2.Upo uhasama kati ya waandishi wa habari wa Iringa na Polisi? -- Ndiyo.
    3. Ipo orodha ya waandishi watatu wa kushughulikiwa? -- Haipo.
    4. Nguvu zilizotumika zilizidi kiasi? -- Hapana.
    5. Upo utaratibu wa vyama vya siasa kukata rufaa kama visiporidhika na maamuzi ya Polisi? -- Hakuna.
    6. Kuna tatizo la mahusiano kati ya polisi na vyama vya siasa? -- Hakuna.

    Sasa haya maswali kweli unaweza kuyaundia kamati ya "ushauri"?

    In a case like this, you as a minister, you are not supposed to take a "subjective" route but rather an "objective" one. There is no object in your quest sir, only subjects. Nothing you will find out sir and even if you find something, you won't take any measures because: in your findings there will be no object. Subjects cannot be offenders but can only be offended. Kalaghabhao!

    ReplyDelete
  5. Tatizo la serikani ya CCM mnakurupuka kujibu hoja za CHADEMA na ndio maana mnaonekana hamna jipya. Kuhusu hili ningetegemea Serikali kutoa tofauti kati ya Kamati na Tume ili wananchi na husasan wale wa kaiwada waweze kuwaelewa....kuwe makini na sio kujitetea....Polisi hawajatoa repoti ya Tume ya Dr. Ulimboka, Tume ya Morogoro, na sasa ni Tume/Kamati Iringa...je zina tija?

    ReplyDelete
  6. mwanasheria mkuu wa serikali hufanyi wajibu wako. mpaka waziri anaumbuka? idara za sheria wizarani zinanfanya nini?
    Viongozi tafuteni ushauri wa kisheria kable ya kufunguka. ona sasa. aibu tupu. huyu msemaji nae katia chumvi kenye jeraha. mauaji yanaundiwa kamati? Yamakuwa sendi off au harusi.
    NI MUHIMU NA LAZIMA KIUNDWE CHOMBO CHA KUSIMAMIA VYOMBO VILIVYOPEWA KAZI YA KULINDA MALI, MAISHA NA HAKI ZA WATANZANIA.
    Na ninyi waandishi, mpaka afe mwenzenu ndo mlivalie njuga? si ubaguzi na matumizi mabaya ya vyombo vya habari? nilitehemea muwasemee wale wasio na pa kusemea. mmenisikitisha kwa kweli. mmekosa hadhi ya kuwa mhimili.
    Na ninyi wanaharakati, hamna haja ya kwenda kuishtaki serikali nje. wapelekeni kwenye mahakama ya katiba kwani wameshindwa kusimamia haki ya msingi ya kuishi kwa mtanzania. mshtakiwa wa kwanza mwanasheria wa serikali, pili waziri wa mambo ya ndani, tatu IGP kny ya wenzake wote akina Chagonja, RPC,RCO wa mikoa yote yalikofanyika mauaji ya raia. Mauaji yote yaorodheshwe wajibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...