Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amesema kuwa ili kuifanya nchi yetu iendelee kuwa salama, kuna haja ya kuwekeza zaidi katika miundombinu ya amani. 

 IGP Mwema ameyasama hayo leo mjini Zanzibar wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi wa kati kwa askari Polisi kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi mjini Zanzibar. Amesema bado kuna haja ya kila mwananchi kuelewa kuwa jukumu la usalama wa nchi hii liko mikononi mwake. 

 Amesema kila mmoja hawezi kukwepa jukumu la kulinda rasilimali yake na mfano mdogo ni pale kila mmoja kwa wakati wake na bila ya kufundishwa pale anapolinda faragha. IGP Mwema pia ameeleza umuhimu wa kwa nini kila Mtanzania anapaswa kuwa mlinzi wa Taifa letu na kutilia mfano kwamba suala la ufalama linaanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, kaya, kijiji, kata ama shehiya tarafa wilaya mkoa na Taifa.

 Amesema katika taaluma ya Polisi, Askari amefundishwa kuwa mlinzi katika mambo manne makubwa ambayo yanamhusi kila mmoja wetu bila ya kujali nafasi yake katika jamii. Mambo hayo ni manne ni fursa ambazo zikiachwa wazi watu wengine wanachukua nafasi ya kuichukua nafasi kuu nne ( four Speces ) sio kama askari lakini hatani kabla ya wa mali wa mali zake, mlinzi wa familia wakiwemo watoto wake pamoja na himaya inayomzunguuka.

 Amewataka Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake, awe mdau wa sualama kama anavyolinda na kuheshimu faragha zake. Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuna haja ya kila kiongozi wa Jeshi la Polisi hapa nchini kuyageuza matazo wanayowakabili kama changamoto na kuzigeuza fursa ya kuleta ufanisi kazini. 

 Naye Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mh. Abdallah Mwinyi, ameelezea mikakati inayochukuliwa na mkoa wake katika kudhibiti usalama wa maeneo mbalimbali na kusema kuwa Ulinzi shirikishi na Polisi Jamii ni jicho la Polisi mitaani. 

Awali akitoa tathmini ya mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Zanzibat ACP Ramadhani Mungi, amesema wahitimu hao wamejifunza mambo mbalimbali ukiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Polisi na vyombo vya Habari. 

Kamanda Mungi, amesema wameweka somo hilo kwa kufahamu kuwa kazi za Polisi zinaingiliana kwa kiasi kikubwa na zile za Waandishi wa Habari na kwamba kila mmoja anamtegemea mwingine ili kufanikisha kazi zake. 

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Kamishna Khalifa Hassan Choum, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Dar es Salaam ACP Ali Lugendo na Maafisa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vikosi vya SMZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sina uhakika kama kichwa cha habari hii kinakasoro, au IGP ndiye aliyekosea. Unapowataka wananchi, maana yake unatoa amri au unawalazimisha. Hakuna kifungu cha sheria ya Tanzania kinachomruhusu mkuu wa jeshi la polisi kuwalazimisha wanachi kufanya kazi ya ulinzi. Maana yake ni kuwa atakayezembea amri hiyo hawezi kuchukuliwa hatua yeyote. Hii inapunguza heshima ya mkuu huyo anapowataka wananchi kulinda nao wakakataa. Anaweza akashauri, lakini siyo kuwataka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...