JUMLA  ya warembo 29 kati ya 30 wanaowania taji la REDDS MISS TANZANIA 2012 leo wameanza ziara rasmi ya kutembelea Vivutio vya Utalii vilivyopo Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Moshi, Arusha na Manyara.

Warembo hao wakiongozwa na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, wakiwa katika mikoa hiyo watatembelea vivutio hivyo na kuhamasisha jamii ya watanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio hivyo vyua ndani na kuhamasisha utalii. 

Pia warembo hao watapata fursa ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na masuala ya utalii. Oktoba 7, warembo hao watatembrelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, katika lango kuu la kupandia Mlima huo la Marangu. 

Aidha kwa mujibu wa ratiba hiyo, inaonesha kuwa warembo hao watafanya tamasha la Michezo mjini Arusha kabla ya kuelekea Monduli ambako Oktoba 8 watazuru Kaburi la Waziri Mkuu wa Zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hivo yupo yeyote jati ya hao mabinti mwenye nywele zake za kuzaliwa?

    ReplyDelete
  2. Hilo basi halina mikanda (safety belts)? Mambo mengine jamani hata huyu Mungu wetu inabidi tumpe msaada, isije kuwa taabu hapo mbele na kubaki kusema mapenzi yake Mungu!!!!...

    ReplyDelete
  3. Miss Tanzania ijayo TUNATAKA MWAKILISHI MWENYE UTANZANIA HALISI KUANZIA NYWELE!

    NAUNGANA NA MDAU WA KWANZA HAPO JUU ANONYMOUS WA Sun Oct 07, 01:34:00 PM 2012

    ILI KULINDA ASILI YETU KINASABA TUNAHITAJI UPIMAJI WA DAKITARI KUHUSU MAUMBILE (DNA na chembe asilia) YA WASHINDANI WA UREMBO IKIWEMO NYWELE ASILIA NA VINGINEVYO IWE NI KIGEZO ILI KUMPATA MISS HALALI!

    BADALA YA KUWAKILISHWA NA FOTO KOPI YA MCHINA KWA NYWELE AU MAKALIO , KOPE AMA NYUSI!

    SWALI:
    TUJIULIZE KWA NINI MARA ZOOOTE HATUFUZU KWENYE MASHINDANO YA DUNIA?

    JIBU:
    NI VILE TUNAPELEKA WASHINDANI WASIOKUWA ASILIA KWA UZURI KWENYE MASHINDANO YA DUNIA INGAWA KTK MASHINDANO VIGEZO VINGINE ZAIDI YA UZURI HUZINGATIWA PIA!

    ReplyDelete
  4. Ahsante kwa aliyouliza kuhusu kuna hata mwenye nywele zake, labda yule Fatuma Ramadhani lakini wote na minwele ya bandia, mavazi ya kigeni nadhani na ngozi za kuchubiliwa, huu sio u-Tanzania, acheni kuigaiga. Hebu fanyeni mashindano ya urembo umkiwa hasa Watanzania na asili yetu. Watu wapo katika kutafuta Vazi la Taifa ndio tutavaa na minywele kama wahindi/wazungu n.k. Aibuuuu.

    ReplyDelete
  5. Warembo nani kasema uzuri ni lazima uwe na manywele?

    Nani kasema ukikosa nywele kanunue za Mchina?

    Kama mngechagua kunyoa vipara baada ya kuona nywele ni mgogoro kwenu tungekuwa pamoja kwa kuwa miongoni mwa jamii yetu ya Ki-Tanzania wanawake wa Kabila la Kimasai hunyoa nywele na wanatoka chicha!

    Kwa nini msionane na dada yenu Flaviana Matata ili awafundishe kujiamini mkiwa na vipara?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...