Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Gavana
Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson na
viongozi wa serikali ya nchi hiyo katika jumba la Rideau jijini Ottawa,
Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili
jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku akiangaliwa na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa,
Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4,
2012.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa
Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya
siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi katika viwanja vya jumba
la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya
ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba
hilo ndilo makazi na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia
mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa
kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni
mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za
kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Jaman watu wa protokali mbona mnamfanyia hv raisi wetu?.kweli mnaanda ziara ya yeye kupokelewa na waziri wa mambo ya nje?hv mnajua uzito wa cheo cha rais wa nchi?hv kweli kiongozi mkuu wa canada akija tz anaweza kupokelewa na waziri Membe kweli?.watu wa protokali kuweni na heshima na rais wetu maana ninyi ndio mnaopanga hizi safari..Mh rais wangu JK siku nyingine usikubal kwenda kwenye hizi ziara ambazo haupokelew na watu wa level yako.
ReplyDeleteMdau Toronto
We mdau wa Toronto hapo juu,usitutie aibu. Mhe, amepokewa rasmi na gavana wa canada ambaye anamuwakilisha malkia katika nchi hiyo unayoishi wewe.muulize michuzi akupe habari zaidi mimi nimeona kwenye luninga mapokezi rasmi.
ReplyDeleteCha ajabu kuhusu Canada: Prime Minister (mtendaji mkuu wa serikali kitaifa) anateuliwa na wananchi kupitia sanduku la kura. Kisha yeye anapendekeza kwa Malkia wa Uingereza jina la atakayekuwa Governor General na Malkia anampitisha. Governor General anakuwa na nguvu kubwa hata kumshinda Prime Minister kwa vile anamuwakilisha Malkia moja kwa moja, ambaye ndiye mwenye dola ya Canada. Ajabu la tisa na nusu la dunia.
ReplyDeleteBig up Anony wa misho Fri Oct 05, 07:59:00 AM 2012.
ReplyDeleteHii ni ajabu kweli..