Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Bi. Regina Kikuli akipokea mashine hiyo kutoka kwa Naibu Kamishina na Kiongozi wa Ujumbe wa Watu wa China hapa nchini,Bw. Ji Junfu uliotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mashine iliyokabidhiwa ambayo ina thamani shilingi milioni 131,970,000

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetoa msaada wa mashine yenye thamani ya shilingi milioni 131,970,000 kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili itakayotumika kutoa huduma za kutambua maelezo na takwimu za mgonjwa, kutambua sauti na picha ya mtaalamu na mgonjwa na hivyo kurahisisha mawasiliano.

Mfumo wa mashine hiyo ni kufanya uchunguzi wa kina ambapo mgonjwa analaza viganja vya mikopno yake miwili na hivyo mashine hiyo inaweza kutambua hali na maendeleo ya mgonjwa kwa kuonyesha moja kwa moja ugonjwa gani anaoumwa mgonjwa. Mashine hii pia itaunganishwa na mtandao wa intaneti ambapo watalaamu waliopo Muhimbili wataweza kuwasiliana na watalaamu walioko chini China ili kutoa huduma kwa wagonjwa kupitia njia ya masafa (telemedicine).

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Regina Kikuli aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa msaada huo na kuwaomba kuendeleza ushrikiano huo. Bi. Kikuli alisema Hospitali ya Taifa Muhimbili ihakikishe inatumia fursa hii vizuri kwa kutoa mafunzo kwa wataalamu wetu namna ya kuitumia mashine hiyo na kuielewa tiba asilia ya kichina.

Aliongeza kuwa Hospitali ihakikishe inafunga mashine hiyo katika sehemu nzuri, itumike kwa uangalifu na kuwa na mpango mahususi wa matengenezo ya mara kwa mara na hivyo kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu.

Aliutaka uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuongeza vyumba vya huduma na mafunzo na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uwepo wa huduma ya tiba asili ya Kichina.

Akikabidhi mashine hiyo, Naibu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Ji Junfu, alisema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa wananchi wake.

Uhusiano wa tiba za kichina kati ya Tanzania na China ulianza miaka ya 1980 ambapo mwaka 1987 Mwalimu Nyerere alimuomba Kiongozi wa China wakati huo Deng Xiaoping kutuma watalaamu wa tiba nchini kwa ajiri ya kutibu wagonjwa wa HIV/AIDS.

Bw. Junfu alisema katika miaka 50 iliyopita Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetuma madaktari zaidi ya 2,000 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za Zanziba pamoja na zile za Mikoa ili kutoa huduma za tiba asilia za kichina.

Miaka mitatu iliyopita, Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, ilitoa msaada Shilingi Bilioni 16.22 kwa ajiri ya ujenzi wa Taasisi ya Upasuaji Moyo iliyojengwa ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbli ambapo Serikali ya Tanzania katika ujenzi huo imechangia kiasi cha shilngi Bilioni 6 kukamilisha ujenzi na ufungaji wa vifaa tiba. Ujenzi wa taasisi hiyo umekamilika na jengo hilo litafunguliwa wakati wowote kuanzia sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...