Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sherehe za  Siku ya Familia ‘Familiy Day’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhusisha wafanyakazi  wa benki  hiyo na familia zao.
 Baadhi ya wanafamilia wakiwa katika Siku ya Family Day

Sehemu ya Burudani kwa Watoto.

DAR ES SALAAM, Tanzania

WATANZANIA wametakiwa kupanua wigo wa maendeleo yao kiuchumi, ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia na taifa, kwa kujiunga na kutumia ipasavyo huduma ya ‘SimBanking’ inayotolewa na Benki ya CRDB

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk Charles Kimei, wakati wa sherehe za kila mwaka za Siku ya Familia ‘Family Day’ inayohusisha wafanyakzi wa benki hiyo na familia zao, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kunduchi Welt ‘n’ World’ jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa, kila mwaka wa sherehe hizo huwa na huduma moja inayotangazwa, ambapo mwaka huu kipaumbele ni huduma ya ‘SimBanking’ iliyozinduliwa Aprili, ikiwa na lengo la kurahisisha maisha ya wateja na kuwapa fursa ya kuachana na ukiritimba wa kupata huduma za benki kwa kupoteza muda mwingi kwenye foleni.

Aliongeza kuwa, huduma hiyo ni ya kipekee miongoni mwa mabenki nchini, inayoweza kuchangia upanuzi wa maendeleo ya kielimu, kiuchumi na kijamii, kwa kumpa fursa mteja kuhamisha fedha kwenda akaunti yoyote ndani ya mtandao wa CRDB.

“Huduma hii inasaidia huhamisha fedha kwenda kwenye simu ya mkononi ya mtandao wowote nchini, kulipia ankara (bili) mbalimbali, kununua muda wa maongezi kwa mitandao yote chini, kununua umeme wa LUKU, kutuma na kuchukua fedha kwenye ATM bila kadi ya benki hata kama aliyetumiwa hana akaunti ya benki hiyo,” alisema.

Akizungumzia sherehe hizo, Dk Kimei alisema kuwa ‘Family Day’ husaidia kuwaweka pamoja wafanyakazi na familia zao, ili kuzungumza, kujifunza, kubadilishana mawazo, kuimarisha ushirikiano miongoni mwao, jambo ambalo haliwezi kufanyika kirahisi kutokana na mgawanyiko wa matawi na ofisi zao.

Aidha, aliongeza kuwa, kwa miezi 11 ya mwaka huu wameweza kuajiri zaidi ya wafanyakazi 700 na kufanya orodha ya waajiriwa katika benki hiyo kuongezeka zaidi, ambapo ujazo wa faida kwa mwaka ukiwa ni asilimia 15, huku akitarajia ongezeko la asilimia hizo kwa Desemba.

“Wastani wa miaka iliyotangulia ya ujazo wa faida ni asilimia 18 hadi 20 kwa mwaka na kutokana na ukweli kuwa hii ni Novemba, tunatarajia ongezo hilo kwa Desemba ili kufikia ama kuvuka kiwango cha miaka iliyopita,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. nini maana ya kuasa? ametuasa au ametuhamasisha?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...