Mtaalam na mshauri aliye kwenye jopo la majadiliano kwa manufaa ya wote ( Smart Partnership) Prof. Lucian Msambichaka akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa mkutano wa kimataifa wa majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership) kwa watanzania. Mkutano huo utafanyika nchini mwezi mei 2013.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushindani la Biashara Tanzania (TNBC) Bw. Samson Chemponda akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa mkutano wa majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership) na namna utakavyowawezesha watanzania kubadilishana uzoefu kutoka kwa wataalam kutoka nchi nyingine kuhusu matumizi ya teknolojia kuondoa umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo kwenye maeneo yao.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye semina kuhusu majadiliano kwa manufaa ya wote ( Smart Partnership) na nafasi ya vyombo vya habari katika kukuza na kuimarisha uchumi na kuongeza uelewa miongoni mwa wananchi kuhusu nafasi na fursa walizonazo katika kukuza uchumi nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa majadiliano ya pamoja utakaofanyika nchini mwezi Mei 2013.
Meneja Mradi wa Majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership) Bi. Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna ambavyo wadau takribani 800 kutoka mataifa mbalimbali watakutana nchini Tanzania kujadili kwa pamoja changamoto za kimaendeleo, kiteknolojia na namna wananchi watanufaika kutokana na kutengeneza mtandao wa kutafuta suluhisho la matatizo ya kiuchumi kutoka pande zilizofanikiwa. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Eh Rose ninakuona ulivyopendeza sana shosti. Hongera kwa mafanikio yako Mwenyezi Mungu anakuongoza na mengi mazuri yatakuja. Wewe ni ngangari bwana. S.C.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...