Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akilaani mashambulizi ya kikundi cha waasi cha M23 kilichoteka mji wa Goma, Mashariki mwa Congo DRC.   Waziri Membe aliyasema hayo alipokuwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano, Wizara ya Mambo ya Nje, mjini Dar es Salaam.  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. John M. Haule na Kushoto ni Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizarani. 
Mhe. Waziri Membe akiongea na Waandishi wa Habari.
Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akitoa msimamo wa Tanzania kuhusu vitendo vya kikundi cha waasi  cha M23 kilichopo Mashariki mwa Congo DRC.  Kushoto ni Balozi Simba Yahya.Picha zote na Tagie Daisy Mwakawago.

Na ALLY KONDO SEIF

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) amelaani kitendo cha kikundi cha M23 kuteka mji wa Goma na kutishia kuteka miji mingine ya Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mhe. Waziri alitoa msimamo huo wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam tarehe 22 Novemba, 2012.

Mhe. Waziri alisema kuwa hali ya usalama mjini Goma ni mbaya kutokana na mashambulizi hayo ya M23 na hali hiyo ikiachwa iendelee, Tanzania itaathirika kwa kiasi kikubwa kwani watu wengi watakimbilia hapa nchini kama wakimbizi.

Aidha, Mhe. Waziri alisikitishwa na kikundi cha M23 cha kupuuza wito uliotolewa na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Sekretarieti ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) wa kusitisha mapigano hayo.

Mhe. Waziri aliendelea kueleza kuwa Tanzania inasikitishwa na jeshi la Umoja wa Mataifa la MONUSCO lililopewa jukumu la kulinda amani Mashariki ya DRC kwa kushindwa kuchukuwa hatua za kukomesha mashambulizi hayo na badala yake kuwa mashuhuda wa mashambulizi yanayofanywa na kikundi cha M23 dhidi ya Serikali na wananchi wa kawaida.

Aliuomba Umoja wa Mataifa utoe mamlaka ili MONUSCO iwe na uwezo wa kisheria wa kukabiliana na waasi wa M23 kama sura ya 7 ya Umoja wa Mataifa inavyoelekeza badala ya kutumia sura ya 6 ya Umoja wa Mataifa inayosisitiza umuhimu wa kulinda amani bila kujibu mashambulizi.

Kuhusu jitihada zinazofanywa na SADC kwa kushirikiana na ICGLR za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo, Mhe. Membe alisema kuwa mwezi Agosti, 2012 Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hizo walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuunda kikosi cha kulinda amani ili kitumwe Mashariki ya DRC. Tanzania iliahidi kuchangia batalioni moja lakini kikosi hicho cha kulinda amani hakijapata ridhaa ya Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa hautaki kutoa ridhaa ili kikosi hicho kipelekwe DRC kwa hoja kuwa tayari jeshi la Umoja wa Mataifa lipo nchini DRC.

Mhe. Waziri alihitimisha Mkutano wake kwa kutoa taarifa kuwa nchi za SADC na ICGLR zitakuwa na mkutano nchini Uganda kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 23 Novemba, 2012 kujadili hatua za haraka za kuchukuwa ili kukabiliana na mzozo wa DRC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Na statement ya mauaji waliyoyafanya waisraeli dhidi ya wakazi wa Gaza ikowapi?

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa Membo pole na majukumu yako ya kila siku,ukiwa bado unaumiza kichwa linakuja suala la
    M23.

    Naomba kutoa ushauri mdogo tu kwako Mheshimiwa.Umekimbilia kwenye suluhisho badala ya kudhibiti chanzo cha UASI-Na hawa si waasi kwangu mimi.Nani anawafadhili hawa M23?(Anafahamika-kikulacho ki nguoni mwako!),pesa wanazipata wapi?Tusikaripie hao `WAASI`,tukaripie anayewafadhili.!

    David V

    ReplyDelete
  3. ASANTE SANA TANZANIA KWA KULAANI MASHAMBULIZI YA M23 KATIKA MJI WA GOMA NCHINI DRCONGO.
    WAAFRIKA LAZMA TULAANI VITA,INARUDISHA MAENDELEO KATIKA BARA LETU.
    WAZUNGU NA WAARABU HAWEPENDI BARA LETU LIENDELEE,NDO WANALETA UCHOCHEZI TUUWANE WENYEWE KWA WENYEWE.
    /MDAU KUTOKA DRCONGO NA TANZANIA

    ReplyDelete
  4. Too much cable network!

    Hivi Wireless Microphone bei gani?

    Ingawa Tekinolojia ni ghali lakini pana uwezekano angalau tukaenda na wakati na tukapunguza idadi kubwa ya waya za Vipaza Sauti juu ya meza kama inavyoonekana Mhe. Membe akitoa Hutuba.

    ReplyDelete
  5. Nilitegemea pia waziri ataongelea taarifa ya UN kwamba Rwanda na Uganda wanawasaidia M23 halafu wanazishawishi nchi kama yetu zisaidie kupambana na waasi! Ni aibu kwa majirani kushindwa kujua mzizi wa M23! Aibu kubwa.

    ReplyDelete
  6. Je Mh. Membe unajua Uganda nao wanatuhumiaw kufadhili hao waasi? Hamtaweza kufanikiwa kwa sababu takacho panga waasi watakujua siku hiyo hiyo kwakuwa mtakuwa nao kwenye mkutano bila kujua.Jaribu kufikiri kutowahusisha Uganda na Rwanda kwenye mikakati.

    ReplyDelete
  7. Hii vita ni MPANGO WA KIBIASHARA ZAIDI:

    Tuelewe Maslahi ya kibiashara ni kitu kigumu sana ktk maisha yetu, kuna kugeukana na kupanga hila bora mkono wende kinywani.

    Vita inapigwa huku madini yanaibiwa huko Mashariki ya Kongo, hivyo tusiumize kichwa Rwanda na Uganda wapo nyuma ya maslahi ya kibishara ya Madini ya Mashariki ya Kongo huku wakiwa hao hao ndio ndumila kuwili.

    UN haina akili kubaini ktk Ripoti yake yaliyo nyuma ya pazia?

    ReplyDelete
  8. Suluhisho la Vita hii ya Mashariki ya Kongo ni kuzishauri Rwanda na Uganda zibuni njia mpya ya kukabiliana na maisha ama njia mbadala ya mapato badala ya madini ya Kongo!

    ReplyDelete
  9. Bajeti ya US$ 1.4 Bilaion inatoka kila mwaka kwa Majeshi ya MONUSCO kulinda amani eneo hilo.

    Tatizo Majeshi yamesheheni Maafande wa Kihindi na Kifilipino walio kaa kimafao zaidi kuliko kivita, ndio maana hawawezi kazi mbele ya Waasi!

    ReplyDelete
  10. Ugomvi wa DRC na waasi si tu wa M23 hata wa FLDC chanzo chake ni siasa za ndani za DRC. Viongozi wakuu wa DRC ndio wanoujua ugomvi wao na waasi kwa undani,kuna baadhi ya viongozi wa DRC wananufaika na ugomvi huo. Kuwatuhumu Rwanda na Uganda ni kuwatupia lawama ziszo zao. DRC inakosa Siasa safi na Uongozi bora licha ya kwamba ina Watu inao na Ardhi kubwa na yenye rasilimali. Usimamizi wa mambo haya ndio unaosababisha migongano DRC. Hata jeshi letu likienda na kufanikiwa kuwaondoa waasi bado vurugu zitaendelea kwa kuwa DRC hakuna Utawala bora. Hata Rwanda na pia Uganda wakiwekewa vikwazo vurugu zitaendelea. Suluhisho la kudumu la matatizo ya DRC ni kwa AU na UN kuhakikisha kwamba DRC inakuwa na utawala bora.
    JohnJohn

    ReplyDelete
  11. 1. Naunga mkono uamuzi wa Serikali yetu wa kulaani kitendo cha M23 cha kuvamia nchi ya DRC na kuteka mji wa Goma.

    2. Kwa kuwa imethibitishwa na UN kuwa Serikali za Uganda na Rwanda zinawasaidia waasi wa M23 katika uvamizi huo, ni vema Tanzania ikakemea na kulaani kitendo hicho cha nchi hizo mbili.

    3. Ni vizuri pia kwa nchi majirani zinazopenda amani(ikiwamo Tanzania) na kufuata sheria ya kimataifa kuisadia nchi ya DRC katika kulinda mipaka yake. Hatujui kitakachoendela baadaye, iwapo DRC itaanguka.

    4. Vitendo vya nchi hizo mbili vya kusaidia M23 havikubaliki kwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ni vema ikiwa nchi hizo zitasimamishwa uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mpaka zitakapojirekebisha.

    ReplyDelete
  12. 1. Naunga mkono uamuzi wa Serikali yetu wa kulaani kitendo cha M23 cha kuvamia nchi ya DRC na kuteka mji wa Goma.

    2. Kwa kuwa imethibitishwa na UN kuwa Serikali za Uganda na Rwanda zinawasaidia waasi wa M23 katika uvamizi huo, ni vema Tanzania ikakemea na kulaani kitendo hicho cha nchi hizo mbili.

    3. Ni vizuri pia kwa nchi majirani zinazopenda amani(ikiwamo Tanzania) na kufuata sheria ya kimataifa kuisadia nchi ya DRC katika kulinda mipaka yake. Hatujui kitakachoendela baadaye, iwapo DRC itaanguka.

    4. Vitendo vya nchi hizo mbili vya kusaidia M23 havikubaliki kwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ni vema ikiwa nchi hizo zitasimamishwa uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mpaka zitakapojirekebisha.

    ReplyDelete
  13. Bongo ni noma ni maneno ya kulaani, vitendo hamna. Kijana wetu tuliyemlea wenyewe Kabila anahitaji msaada wa kijeshi, kama tulivyofanya zamani kwa mataifa mengine. Waasi wanasaidiwa na Rwanda na Uganda. Tulitakiwa kumsaidia kijana wetu peleka wanajeshi huko, na pia ni nafasi nzuri ya mazoezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...