Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa



  1. Am so inspired what are Tanzanians doing abroad if you just cant help ur fellow Relatives back in Africa??

    Foster Innovations,,,,,, in Tanzania

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza hapo juu, huyu dogo hakai ughaibuni a.k.a abroad ila anaishi nchini Sierra Leone, Afrika ya Magharibi ambapo ndiyo kwao. Alikwenda USA kwa mwaliko.

    Je wewe uliye hapo Bongo una ubunifu gani hapo nyumbani Tanzania uwanufaishe wa-Tanzania na hata ualikwe nje ya Tanzania/
    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  3. What a bright and humble kid.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa pili hapo juu anony wa Fri Nov 23, 04:41:00 AM 2012

    ...Sisi Tanzania tumewekeza kwenye wizi, majungu, rushwa na ubinafsi.

    ...Ubunifu wetu Tanzania ni ktk ubomoaji na sio kujenga hasa kwa wizi, rushwa,majungu na ubinafsi.

    ...Juzi Mdau mmoja akiwachana Wasomi wa Chuo Kikuu Dodoma wakigombea Majoho kwa ajili ya Sherehe za Mahafali na ndio Kipaji cha Mtanzania Msomi hana mchango wowote kwao!!!

    ReplyDelete
  5. ...Tanzania kipaji na uwezo wetu ni kwenye kuiba Mitihani ili kupasi masomo!

    ReplyDelete
  6. Kazi aliyofanya dogo Kelvin Doe wa Sierra Leone hata Engineer au Graduate wa Bongo hawezi!


    TANESCO-Tanzania na Mainjinia wa Mhando mpo, mmemuona dogo vitu vyake?

    ReplyDelete
  7. Ahhh wapi,

    Kipaji na Ubunifu wa Mtanzania ni kwenye TUNGURI na MAJUNGU !

    Hatuna uwezo kama huyu mtoto.

    ReplyDelete
  8. Mambo kama haya hatuna hapa, mtoto akitokelezea kama huyu ukoo unakwepa kumsomesha na ndio kwanza anakabidhiwa sinia la maembe auze badala ya kuandaliwa safari ya Marekani akaonyeshe ujuzi wake.

    Uchawi, Fitina, Roho mbaya na Hirizi ndio Ubunifu pekee wa Tanzania!

    ReplyDelete
  9. Nchini kwao huyu dogo Sierra Leon ndio majuzi tu wametokea vitani, lakni wameweza kumwandaa mtoto akafanya mambo makubwa haya.

    Sisi Tanzania imebaki kukuta mtoto wa umri huo wa miaka 15 akiwa anasoma Sekondari hajui kusoma na kuandika, ktk kujibu maswali ya Mitihani sehemu ya Namba ya Mtihani ndio kwanza anaandika jina lake tena akiwa amelikosea!

    ReplyDelete
  10. Miujiza hii tunaweza?

    Kazi ni kutoa mbinu tu za Kufaulu Mitihani.

    Elimu ya Tanzania tumebaki kukaririsha Wanafunzi kujibu maswali ya Mitihani kwenye Madarasa ya Twisheni!

    ReplyDelete
  11. Aah ah ah ah ah,

    Aah wapi?

    Mtanzania uwezo wake ni kwenye kuunda majini, kumfunga mtu asifanikiwe , kuunda popo bawa na kuruka na ungo!!!

    ReplyDelete
  12. Watoto wa Kibongo kazi ni kudai pesa nyingi wakienda mashuleni na kutega masomo Shuleni,

    Mtoto anaaga kwao kwenda shuleni anashinda Feri akipaa na kukwaruza samaki!

    ReplyDelete
  13. mdau wa pili hivi ulisikiliza habari yote kwa kituo? kweli dogo anaishi siera leone, lakini aliyewezesha kupata huo mualiko ni mserra leone anaishi na kufanya PhD huko USA, na hilo ndilo lililompa moyo mdau wa mwanzo ambaye yupo ughaibuni kufanya kama alilofanya huyo jamaa anaefanya researh yake huko MIT marekani.

    Sasa jiulize wewe mdau wa ughaibuni umefanya nini kuwasaidia vijana wadogo wenye vipaji na ubunifu hapa nyumbani?

    ReplyDelete
  14. Katika umri huo wa miaka 15 kwa watoto wetu wa ki Tanzania unakuta anasoma Sekondari huku:

    1.Akiwa hana hata uwezo wa kisanaa na kiufundi wa kutengeneza angalau upawa kwa kutumia kifuu cha nazi.!

    2.Unakuta haelewi masomo hata moja kichwa chote kimejaa mashairi ya muziki wa Kizazi kipya.!

    3.Hajui kuhesabu sawasawa, kusoma na kuandika, hajui Kiingereza kama Dogo Kelvin Doe wa Sierra Leone anavyomwagika Kimombo hapo,

    Tena kubwa zaidi Dogo wa TZ unakuta anaandika hati mbaya kama bata huku akichanganya herufi kubwa na ndogo!

    ReplyDelete
  15. Mdau wa NO.13 hapo juu anony Fri Nov 23, 03:09:00 PM 2012 UMEMCHANA KAVU KAVU MDAU WA NO.2 WA UGHAIBUNI anony Fri Nov 23, 04:41:00 AM 2012

    ...NI VIGUMU KUPIGA HATUA ZA KIMAENDELEO NCHINI TANZANIA HUKU TUKIWA NA ROHO MBAYA.

    KAMA UNAVYOMCHANA JAMAA YEYE AMEFANYA NINI KUWASAIDIA WATOTO WENYE VIPAJI NCHINI?

    ANAWEZA KUANDAA NE YEYE MWALIKO KUMWEZESHA DOGO YEYOTE MWENYE KIPAJI NCHINI AFIKE HUKO MAJUU ILI KAZI YAKE IONEKANE?

    JIBU, NI SUBUTUUUUU MBONGO NI MBANAJI SANA, KWANZA AKISIKIA HIVYO ATAKATAA ATASEMA HAWAWEZI KUTUMA MWALIKO!!!

    ReplyDelete
  16. Mdau wa Sat Nov 24, 11:23:00 AM 2012: Tuache unafiki na uongo. Jamani wabongo Ughaibuni wengi wasi ngefika huko bila msaada toka wabongo walioko Ughaibuni. Jamaa kibao naowafahamu mie Ughaibuni wamewekeza Bongo na wengi wameliwa na wabongo wasio waaminifu. Tatizo tukiona kitu basi tunafikili ni rahisi tu kufanya. Msione vinahelea vimeundwa. Jiulize waTanzania wangapi wako MIT, Harvad, Oxford na wamefikaje hapo? Ugomvi wa Watanzania ughaibuni unaondeshwa kwenye mitandao ya jamii ni moja ya mawazo mabovu yanayoturudisha TZ nyuma, tubadilike.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...