Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Dkt. Marina Njelekela (kulia walioketi) akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT),Dkt. Hamisi Kibola wakisaini mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la orofa saba la kutolea huduma za wagonjwa binafsi. Anayefuatia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji (UTT) Bw. Gration Kamugisha, Mshauri wa Sheria Mwandamizi wa (MNH) Bi. Veronica Hellar. Waliosimama kutoka kulia ni Bi. Agnes Kuhenga Mkurugenzi Fedha na Mipango wa MNH, Mhandishi Gaudence Aksante Mkurugenzi wa Ufundi MNH, Bw. Mfaume Kimario ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko (UTT) na Bw. Jagjit Singh Mshauri Mwelekezi (UTT).

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) leo wamesaini hati maalumu ya makubaliano ya uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la orofa saba la kutolea huduma za wagonjwa binafsi.

Uchambuzi yakinifu wa mradi huu ulikwishafanyika pamoja na michoro ya jengo hilo ambapo litajengwa katika awamu kuu mbili awamu ya kwanza ikihusisha jengo la wagonjwa wa nje, vyumba vya upasuaji vinne, vyumba vya kulala mtu mmoja mmoja 106.

Awamu ya pili ya mradi huu itajumuisha ujenzi wa vyumba vya kulala wagonjwa wawili wawili 86 na huduma nyinginezo.

Mkataba huo una nia ya kuanzisha mchakato wa kutafuta mfadhili/mwekezaji kutoka katika makampuni na taasisi za kifedha ili kuwezesha ujenzi wa jengo hilo.

Katika mkataba huo UTT ina wajibu wa kuiunganisha MNH na wadau muhimu watakaowezesha upatikanaji wa fedha, usimamizi wa upatikanaji wa mkandarasi pamoja na mshauri mwelekezi katika mradi huo.

Aidha UTT itasimamia shughuli za kila siku za mradi huo kuhakikisha kuwa unafanyika kwa mujibu wa taratibu, kanuni, na sheria ili uweze kukamilika kwa muda na viwango vilivyokusudiwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Dkt. Marina Njelekela alisema ujenzi wa jengo hili utaongeza kwa ufanisi mkubwa utoaji wa huduma katika sekta ya afya hapa nchini kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma na kuongeza uwezo wa Hospitali wa kifedha kuwahudumia watu wenye kipato cha chini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa UTT Dkt. Hamisi Kibola alisema baada ya kukamilika kwa jengo hilo kutawezesha watu wengi wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi kutibiwa hapa Muhimbili na kutawapunguzia gharama za matibabu, usafiri pamoja malazi.

Awamu ya kwanza ya mradi huu itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 17.2

Mshauri wa Sheria Mwandamizi wa (MNH) Bi. Veronica Hellar (kushoto) na Mkurugenzi wa Uwekezaji (UTT) Bw. Gration Kamugisha wakitia saini katika kila ukurasa wa mkataba huo wa uwekezaji.
Mkugenzi Mtendaji wa MNH Dkt. Marina Njelekela (kulia) akikabidhiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa (UTT),Dkt. Hamisi Kibola mkataba wa uwekezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...