Baada  ya kushindwa kufikia dau lililowekwa na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati (Yanga) la kumuuza kiungo wake, Haruna Niyonzima, timu ya El Mereikh ya Sudan imeamua kumwaga dola 75,000 (Shs 120 Milioni ) kumchukua mshambuliaji, Mrisho Ngassa.
 Habari za uhakika zilizoifikia Michuzi Blog zimesema kuwa viongozi wa timu hizo mbili walifikia makubaliano hay oleo na tayari Ngassa ambaye kwa sasa yupo Uganda akishiriki michuano ya Chalenji amepewa taarifa hizo na kukubali kwenda huku Sudan mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.
Taarifa hizo zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Azam FC zilisema kuwa Ngassa alikuwa anaichezea Simba SC kwa mkopo pamoja na timu hiyo kufikia dau la sh Milioni 25 kabla ya kuanza kwa msimu wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Chanzo chetu kimesema kuwa maamuzi ya kumuuza Ngassa ni chanya zaidi kwani wamepita lengo lao la Dola za Kimarekani 50,000 (Sh milioni 80) za hapo awali. Ngassa kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji nyota katika mashindano ya Chalenji na sasa anawania kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao matano.
Awali, El Mereikh ilitaka kumsajili Niyonzima, hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Bin Kleb alisema kuwa walishindwa kukubaliana dau la timu hiyo (Dola 40,000) ni ndogo kulinganisha na thamani ya mchezaji mwenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mrisho.Bidii katika mazoezi na kufuata maelekezo ya mwalimu ni vitu muhimu.Utakutana na changamoto za kugombania namba lakini usikate tamaa.

    David V

    ReplyDelete
  2. Poa sana ,imefika wakati Ngassa kucheza soka la kulipwa nje ya Bongo na kiwango unacho,mwendo huo huo ,ila usibweteke ,kuwa na malengo zaidi ya kucheza ulaya ,umri unakuruhusu bado ,hivyo kaza butu kwa manufaa ya familia yako na taifa stars.Big up ,mdau ughaibuni.

    ReplyDelete
  3. Masikini Mtoto wa Watu. Unaweza kukuta Hata Dola 20000 hana kwenye account yake

    wajanja ndio walao.
    Tunaomba tuonyeshwe mjengo wake?

    ReplyDelete
  4. Watumwa Marekani waliuzwa hivihivi. Mwenye dau kubwa anamchukua yule aliye njemba na mfanyakazi bora mashambani. Hamna tafauti. Huu ni utumwa wa michezo.

    ReplyDelete
  5. Nahisi kuna mchezo unachezwa!!!

    ReplyDelete
  6. Hongera Ngasa. Poleni Simba. AZAM rudini katika misingi yenu ya awali. Siasa chafu za soka zitawaharibia. Kuna watendaji wenu wababaishaji na matapeli wataua mwelekeo wenu.

    Duma
    Dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...