Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Andrew Eriyo akitoa ufafanuzi wa kazi na majukumu mbalimbali ya Tume hiyo kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) wakati alipotembelea banda la Tume hiyo leo (Jumatano Disemba 5, 2012) katika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu zinazoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Amour Kagya (kulia) akigawa nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na machapisho mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo kwa wananchi waliotembelea banda la Tume hiyo leo (Jumatano Disemba 5, 2012) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu Duniani zinazofanyika kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...