Watu  mbalimbali wakiwa wamelizunguka jenereta usiku huu.
 Pichni ni mwanamuziki kutoka DRC-Congo,JB Mpiana akitumbuiza jukwaani mara baada ya kupanda mnamo majira ya saa tisa kasoro,baada ya hitilafu za umeme kwenye jenerata kurekebishwa.

SHOO YA UZINDUZI WA ALBAM YA PILI YA MASHUJAA BAND,YASHINDWA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB USIKU HUU KUTOKANA NA KATIZO LA UMEME LA MARA KWA MARA LINALOSABABISHWA NA JENERETA LINALOTUMIWA KUTOA UMEME KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,JIJINI DAR.

HALI HIYO IMEPELEKEA MMILIKI WA BENDI YA MASHUJAA,MAMA SAKINA KUPOTEZA FAHAMU NA KUKIMBIZWA HOSPITALI.

HADI SASA HAIJAFAHAMIKA KUWA HALI YAKE IKO VIPI KWANI HAKUNA TAARIFA ZOZOTE JUU YAKE.

MAFUNDI BADO WANAENDELEA NA MAREKEBISHO YA JENERETA HILO NA IWAPO LITAKAA SAWA,BASI NI MOJA KWA MOJA BENDI YA WENGE BCBG NDIO ITAPANDA JUKWAANI,CHINI YA MKONGWE JB MPIANA.

TUTAENDELEA KUJUZANA KADRI MAMBO YATAKAVYOKUWA YAKIENDELEA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mamaa Sakina pole na Masahibu yaliyokufika!

    Hiyo ndiyo hali yetu, (Waswahili) tunatumia sana jitihada kukabiliana na wenza badala ya (Wenzetu kwingineko) hukabiliana zaidi na hali halisi!

    Mifano :

    1.Msituni Wanyama hugopa zaidi binaadamu badala ya wenyewe kwa wenyewe wanyama.

    2.Wenzetu kwingineko wanakabiliana zaidi na hali halisi mfano mifumuko ya bei, ushindani wa kibiashara kwa njia huria na matatizo ya kiuchumi.

    3.Sisi Waswahili hapa Ndo ndo ndo kwa Fundi Baisikeli Mibuyu saba tunakabiliana zaidi na kuogopa watu wenzetu kama ilivyo msituni wanyama wanavyoogopa watu!

    ReplyDelete
  2. Mhhhhh!,

    Sio bure litakuwa ni 'DUMANGO' tu!

    ReplyDelete
  3. Ahhh!,

    Kwa kweli 'Sayansi' ina nguvu sana!, sio mchezo hadi jenereta imekataa kuwaka?

    ReplyDelete
  4. Ohooo , enhhhh!

    Jenereta imekataa kuwaka?

    ReplyDelete
  5. Jenereta ilipokataa kuwaka, je kwa nini hamkumwita Dr. Manyaunyau?

    ReplyDelete
  6. Makubwaa!

    Chuma Jenereta kimezidiwa na uwezo wa Sayansi ya Jadi?

    ReplyDelete
  7. Amakweli kuna 'watu' na 'viatu' !

    Ni bora kuwahi makazi ya milele kwa Mwenyezi!!!

    Maisha tunayoishi tunanusurika na Msaada wa Mwenyezi, laiti tungekuwa tunafahamu yaliyomo mioyoni miongoni mwetu kweli Dunia ingekuwa mahala pa kuendelea kuwepo???

    ReplyDelete
  8. EEEEH???? MBONA KILA MTU ANAONGELEA MAMBO YA UTAMADUNI? MNATAKA KUSEMA MASHUJAA BAND WALIPIGWA DAFRAU ILI WASIPERFORM??? BY THE WAY VP JB MPIANA SHO YAKE ILIKUA POA AU???? (( KWA WALE MLIOENDA)) SHUKRAN

    ReplyDelete
  9. Sayansi ingetumika kwa Tija, nafikiri tungefanikiwa sana nchini.

    Tatizo ni mwelekeo wake unalenga zaidi kubomoa kuliko kupiga hatua!

    ReplyDelete
  10. Ni ajabu na kweli!

    Hapa ndio unashuhudia mtu anauwezo wa kuuzima moto kwa kujamba!

    ReplyDelete
  11. Kuna njama zimetumika kumuangusha huyo muandaaji wa shoo zote hizo! Wanajulikana sana wale wanaojifanya mabingwa wa shoo! Usipowashirikisha katika shoo yako ujue watakuvurugia kwa njia yoyote ile! Wanajulikana sana hao. Hata wasanii wasioshirikiana nao hawapigi nyimbo zao kwenye radio yao! Maendeleo hayawezi kuja kwa njia hii!

    ReplyDelete
  12. Mlikosea sana mlipoona mambo sio mambo mngemwita 'Mkuu wa Idara hiyo' Dr. Manyaunyau aje kuiwasha jenereta tokea saa 2 usiku watu wangeburudika kwa masaa yote 7 hayo, badala ya kutumia jitihada za Kiufundi za kawaida zilizowezesha iwake saa 9 usiku!.

    Si mnaona mlivyo wagharimu Wapenzi masaa 7 yote hayo nje ya burudani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...