Watu mbalimbali wakiwa wamelizunguka jenereta usiku huu.
Pichni ni mwanamuziki kutoka DRC-Congo,JB Mpiana akitumbuiza jukwaani mara baada ya kupanda mnamo majira ya saa tisa kasoro,baada ya hitilafu za umeme kwenye jenerata kurekebishwa.
SHOO YA UZINDUZI WA ALBAM YA PILI YA MASHUJAA BAND,YASHINDWA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB USIKU HUU KUTOKANA NA KATIZO LA UMEME LA MARA KWA MARA LINALOSABABISHWA NA JENERETA LINALOTUMIWA KUTOA UMEME KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,JIJINI DAR.
HALI HIYO IMEPELEKEA MMILIKI WA BENDI YA MASHUJAA,MAMA SAKINA KUPOTEZA FAHAMU NA KUKIMBIZWA HOSPITALI.
HADI SASA HAIJAFAHAMIKA KUWA HALI YAKE IKO VIPI KWANI HAKUNA TAARIFA ZOZOTE JUU YAKE.
MAFUNDI BADO WANAENDELEA NA MAREKEBISHO YA JENERETA HILO NA IWAPO LITAKAA SAWA,BASI NI MOJA KWA MOJA BENDI YA WENGE BCBG NDIO ITAPANDA JUKWAANI,CHINI YA MKONGWE JB MPIANA.
TUTAENDELEA KUJUZANA KADRI MAMBO YATAKAVYOKUWA YAKIENDELEA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.
Mamaa Sakina pole na Masahibu yaliyokufika!
ReplyDeleteHiyo ndiyo hali yetu, (Waswahili) tunatumia sana jitihada kukabiliana na wenza badala ya (Wenzetu kwingineko) hukabiliana zaidi na hali halisi!
Mifano :
1.Msituni Wanyama hugopa zaidi binaadamu badala ya wenyewe kwa wenyewe wanyama.
2.Wenzetu kwingineko wanakabiliana zaidi na hali halisi mfano mifumuko ya bei, ushindani wa kibiashara kwa njia huria na matatizo ya kiuchumi.
3.Sisi Waswahili hapa Ndo ndo ndo kwa Fundi Baisikeli Mibuyu saba tunakabiliana zaidi na kuogopa watu wenzetu kama ilivyo msituni wanyama wanavyoogopa watu!
Mhhhhh!,
ReplyDeleteSio bure litakuwa ni 'DUMANGO' tu!
Ahhh!,
ReplyDeleteKwa kweli 'Sayansi' ina nguvu sana!, sio mchezo hadi jenereta imekataa kuwaka?
Ohooo , enhhhh!
ReplyDeleteJenereta imekataa kuwaka?
Jenereta ilipokataa kuwaka, je kwa nini hamkumwita Dr. Manyaunyau?
ReplyDeleteMakubwaa!
ReplyDeleteChuma Jenereta kimezidiwa na uwezo wa Sayansi ya Jadi?
Amakweli kuna 'watu' na 'viatu' !
ReplyDeleteNi bora kuwahi makazi ya milele kwa Mwenyezi!!!
Maisha tunayoishi tunanusurika na Msaada wa Mwenyezi, laiti tungekuwa tunafahamu yaliyomo mioyoni miongoni mwetu kweli Dunia ingekuwa mahala pa kuendelea kuwepo???
EEEEH???? MBONA KILA MTU ANAONGELEA MAMBO YA UTAMADUNI? MNATAKA KUSEMA MASHUJAA BAND WALIPIGWA DAFRAU ILI WASIPERFORM??? BY THE WAY VP JB MPIANA SHO YAKE ILIKUA POA AU???? (( KWA WALE MLIOENDA)) SHUKRAN
ReplyDeleteSayansi ingetumika kwa Tija, nafikiri tungefanikiwa sana nchini.
ReplyDeleteTatizo ni mwelekeo wake unalenga zaidi kubomoa kuliko kupiga hatua!
Ni ajabu na kweli!
ReplyDeleteHapa ndio unashuhudia mtu anauwezo wa kuuzima moto kwa kujamba!
Kuna njama zimetumika kumuangusha huyo muandaaji wa shoo zote hizo! Wanajulikana sana wale wanaojifanya mabingwa wa shoo! Usipowashirikisha katika shoo yako ujue watakuvurugia kwa njia yoyote ile! Wanajulikana sana hao. Hata wasanii wasioshirikiana nao hawapigi nyimbo zao kwenye radio yao! Maendeleo hayawezi kuja kwa njia hii!
ReplyDeleteMlikosea sana mlipoona mambo sio mambo mngemwita 'Mkuu wa Idara hiyo' Dr. Manyaunyau aje kuiwasha jenereta tokea saa 2 usiku watu wangeburudika kwa masaa yote 7 hayo, badala ya kutumia jitihada za Kiufundi za kawaida zilizowezesha iwake saa 9 usiku!.
ReplyDeleteSi mnaona mlivyo wagharimu Wapenzi masaa 7 yote hayo nje ya burudani?