Changchun, Jilin,China
Elimu Maalum kuhusu Uzalendo inabidi itolewe ili kuwafanya watanzania
waendelee kuheshimu Uhuru na dhana nzima, hayo yalisemwa na
wachangiaji kwenye mjadala mfupi ulioandaliwa ili kuadhimisha miaka 51
ya Uhuru wa Tanzania hapa.
Mjadala huo mfupi, uliofanyika katika Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou
Wang jana (Jumapili), ulikuwa umeandaliwa na watanzania wanaoishi
hapa, ambao wengi ni wanafunzi kwenye Vyuo Vikuu mbalimbali vilivyopo
kwenye jimbo hili.
Walisema kuwa elimu ya Uraia imeonyesha mapungufu makubwa kwa kuwa
haiwafanyi vijana kuwa na uzalendo kwa nchi yao, kama ilivyokuwa
mwanzo. Walipendekeza kuwa watengenezaji wa mitaala waangalie
utengenezaji wa elimu hiyo katika changamoto za uchumi wa soko huria,
ambalo linapingana kwa kiasi kikubwa na dhana ya uzalendo.
Walionya kuwa hata mmomonyoko wa maadili na ubinafsi unaolisumbua
taifa kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa elimu hiyo ya Uzalendo.
Wachangiaji Wakuu walikuwa Yazidu Saidi, Hamza Ibrahim, Captain Mwita
Vedasto Wambura, Tessua Ally na Albert Memba. Mjadala huo uliratibiwa
na Innocent Mugisha.
Watanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa Changchun,
Jilin, China wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mjadala mfupi wa
maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa
Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili.
Mchangiaji Yazidu Saidi akizungumza kwenye mjadala mfupi wa
Maadhimisho ya Miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye
Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili.
Mwita Vedasto Wambura akichangia kwenye mjadala wa
maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa
Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili.
Mchangiaji Hamza Ibrahim akichangia kwenye mjadala mfupi wa
maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa
Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili.
Wanajamii, tusikidanganye kizazi kipya au kinachofuatia. Tanzania haijawahi kutawaliwa na wageni, hivyo haijapata uhuru 1961. Iliyopata uhuru 1961 ni Tanganyika au kwa jina jengine la sasa ni Tanzania Bara. Tanzania ni Jamhuri ya muungano wa nchi za Tanganyika iliyopata uhuru wake 1961 na Zanzibar iliyopindua 1964. Tanzania iliunda 1964. Hivyo si sahihi kuandika Tanzania inasheherekea uhuru wa miaka 51.
ReplyDeleteMbona Wanaume watupu? Wanawake wapo wapi?
ReplyDeletegeneder haikizingatiwa ktk mjadala
ReplyDeleteUzalendo utachangiwa na mchakamchaka, sanaa, utamaduni, mafunzo ya historia ya kweli ktk shule zote za msingi na sekondari binafsi na za serikali.
ReplyDeleteUhuru maana yake nini? au ni kutoka chini ya utawala wa kizungu na kuwa chini ya utawala wa wachache wa waafrika wenzetu?
ReplyDeleteWanazidi kuwa matajiri wao na watoto wao kila kukicha wakati mamilioni tunazidi kuwa 'makapuku'
Tafakari! Tuchukue Hatua!
HAWA WAKO WAPI?DODOMA AU KCMC?
ReplyDeleteWako kishumundu kwani huoni migomba na kahawa kwenye background?
ReplyDelete