Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), (kushoto) akisalimiana na Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa Madagascar mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Januari, 2013. Mhe. Rais Rajoelina yupo nchini  kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano unaoendelea wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA).
Mhe. Rais Rajoelina akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili.
Mhe. Rais Rajoelina akiwa amefuatana na Mhe. Membe mara baada ya kupokelewa.
Mhe. Rais Rajoelina akipita katikati ya Gwaride  lililoandaliwa kwa heshima yake huku akisindikizwa na Mhe. Membe
Mhe. Rais Rajoelina akiwa na Mhe. Membe wakifurahia burudani ya ngoma za utamaduni zilizokuwepo Uwanjani hapo mara baada ya kuwasili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Aisee Rais Mtoto kabisaaa, alafu uniambie eti mzee wa miaka 60 kwenda 70na huko anataka kugombea uraisi? hatutaki wazee saivii kwanza wanaongoza kuchapa usingizi tuu hawapo makini hata madereva wazee sio makini sio wazuri kabisa,nguvu ya vijana tu hata akiwa na miaka 28 .

    ReplyDelete
  2. Huyu bwana mdogo bado hata ananuka maziwa hakafu ndo anaongoza Nchi! sasa yeye hata hajui mambo ya itifaki, mwanajeshi anampigia saluti yeye anampa mkono! wajameni Mweeeee.

    ReplyDelete
  3. SIASA KITU CHA AJABU,HUYU MEMBE ALISHA MUITA HUYU JAMAA DISCO JOKER LEO ANAENDA KUMPOKEA AIRPORT NA ZULIA JEKUNDU

    ReplyDelete
  4. Kwani hamjui kuwa huyu ni DJ madhuhuri na mtaalam, nashangaa ma D J wazalendo hawajihusishi na siasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...