Tafadhali pokea taarifa hii kuhusu uwezekano wa matukio ya Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku) katika baadhi ya maeneo ya mikoa  ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara  na maeneo jirani ya mikoa hiyo kati ya tarehe 30 Januari, 2013 hadi 01 Februari, 2013. 
Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo tajwa.
 
Ahsante

Public Weather Service,
 Tanzania Meteorological Agency.
Ubungo Plaza,
Morogoro Road, P.O.Box 3056,
 Dar es Salaam:
Tel: +255 22 2460706-8;Fax: +255 22 2460735
 :Website: www.meteo.go.tz 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Watanzania sisi tumerogwa na nani? Yaani hata TMA wanatoa ramani ambayo inaonyesha ziwa Nyasa lote liko upande wa Malawi! Mbona hata hiyo kesi tumekwishashindwa hata kabla haijaanza?

    ReplyDelete
  2. Wewe mdau ni mbwiga kweli hv hiyo ramani inaonesha maziwa kitulize Kama hauna la kuchangia watu wanatoa taarifa nyingine nawe unatumbukiza vitu tofauti uende na wakati

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Kwanza Kesi hiyo Ushindi upo, kwa kuwa Mhe.Dr.Aleck Che-Mponda Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu yupo Marekani kwa balozi wetu wa UN amepeleka THEIS YAKE YA PhD. ambayo ilizungumzia mzozo wa Ziwa na ukweli wa kuwa Sheria ilikwisha tolewa na huyohuyo Mkoloni wetu sisi na Malawi yaani Mwingereza mwaka 1924 ya kuwa Mpaka wetu unapita katikati ya Ziwa Nyasa!

    ReplyDelete
  4. Haya kwakuruka!

    >Mguu pande!

    <(Moja)!

    >Mguu sawa!

    <(Moja mbili tatu moja)!

    HIVYO NDIVYO WAKAZI WA MABONDENI WANAVYOELEKEA KUPOKEA MAELEKEZO KUTOKA MAMLAKA YA USIMAMIZI YA HALI YA HEWA, KUHUSU KUKAA KWA TAHADHALI KULINGANA NA DALILI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA YANAYOTARAJIWA PUNDE!

    Sio muone angalizo hili muanze dharau zenu?,

    Ohooo Shule zimesha funguliwa hakuna pa Hifadhi na Mabwe Pande Kumejaa, tunataka tuwaweke Madiaspora wanaorudi kutoa Majuu waliopigika kama Ugiriki!!

    ReplyDelete
  5. WAMEONYESHA WAPI WE JAMAA AU MIE SINA MACHO HAPO.OK WADAU ANGALIENI NANYI PIA

    ReplyDelete
  6. Mdau wa kwanza mimi sioni ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa wala Bahari ya Hindi naona picha ya setelaiti ikionesha mawingu na mkusanyiko wa Kimbunga 'Fellani wa Everton'.

    Hata hivyo shukrani kwa taaarifa sisi wavuvi Ferry Kigamboni tutazingatia angalizo la idara ya hali ya hewa.

    Mdau
    Nahodha wa Dau
    Kigamboni.

    ReplyDelete
  7. Kweli zimeanza huku kifujo fulani Tukuyu.
    Suala la ramani muhimu. Ni uzembe kwa taasisi ya serekali kuonyesha ramani ambayo haitambuliwi na serkali, some disciplinary action should follow.

    ReplyDelete
  8. Mzaha mzaha hutumbua usaha,

    Ni muhimu kuwajibishana kwa makosa madogo madogo kama haya mabayo yanaweza kutugharimu sana, endapo Malawi wataona wanaweza kutumia nafasi hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...