Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Zahanati ya Guluka Kwalala iliyopo katika Halmashauri yake baada ya kuwasili kwa ajili ya kumpongeza Mkazi wa eneo hilo kwa kujifungua Salama mtoto wa Kwanza katika Wodi ya Wazazi aliyoijenga kwa nguvu zake kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo ikiwa ni kutekeleza katika moja ya ahadi alizozitoa kwa wapiga kura wake.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia na kumpongeza Bi. Halima Abubakari aliyejifungua mtoto wake katika Zahanati G/Kwalala iliyojengwa na Mstahiki Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa amepakata mtoto wa Bi. Halima Abubakary mkazi wa Kata ya Gongo la Mboto katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala aliyejifungua salama usiku wa kuamkia Machi 19, 2013 kwenye Zahanati iliyojengwa na Mstahiki Meya ikiwa ni kutekeleza ahadi zake kwa wapiga kura wake.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimchekesha mtoto huku akiwa ameshikilia zawadi ya mtoto kwanza kuzaliwa kwenye Zahanati yake.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika wodi ya wazazi iliyopo kwenye Zahanati ya G/Kwalala.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwasogezea huduma za Afya karibu na makazi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. WAGONJWA WAPEWE SARE ZA HOSPITALI!

    ReplyDelete
  2. Huyu kijana atayarushwe kuwa RAis jamani ni mchapakazi ila asilewe sifa na asiharibiwe maana kishaingizwa kwenye CC ya CCM JErry, tafadhal uwe na uzi huo huo nakuahidi kura yangu ya Urais pindi utakapochaguliwa na nitahamasisha na wengine unafaa endelea hivo hivo

    ReplyDelete
  3. Simply brilliant......Congrats Hon. Jerry!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana endeleza utaifa huo na kuwapa masoma na wengine taifa liwe la kukubalika na si machafuko kwa kile kinachotangazwa kwamba serikali haijafanya halafu kuhamasisha maandamano huku kazi kama hizi zinalala.Tazama hata unavyorenba jiji na ubunifu wa hali ya juu,tayari ajira kwa vijana.Si vibaya nikitoa ushauri kuhusu uchafuzi unaojitokeza kutokana na biashara holelela kwani zinapangwa hadi barabarani na hatari ya ajali kwa vyombo na binadamu watumiao barabara si kwa Ilala pekee bali mkoa wote .Tafadhali kutaneni wadau ili uamuzi usiwe wa eneo moja bali lifanyike kwa kutumia kanuni zitakazotekelezeka na uwajibishwaji kwa watakaokabidhiwa uangalizi uzingatiwe bila kumumunya.
    Ni hatari sana japo wapo wasemao hiyo ni ajira,lakini ni sawa vile ambavyo huwezi kuandaa chakula bandani mwa mifugo.
    Liangalieni hili kitaifa na si kisiasa tafadhali.

    ReplyDelete
  5. I love this guy. God bless you uje kuwa rais wetu.

    ReplyDelete
  6. anonymuos no 1 pendekeza namna ya kupata sare za wagonjwa kijana Jerry kahamasisha nakujenga na hata kusimamia miundo mbinu iliyopo sitashangaa kufanya usafi wakamlamu ukikutana na uchafu baada ya ufunguzi leo.Hima wananchi tusimame pamoja kwa kushiriki.

    ReplyDelete
  7. Bravo Hon. Jerry Slaa

    ReplyDelete
  8. Keep it up! Wengine nao waige mfano wako kaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...