Na Abdulaziz Lindi 
Kijana Ismai Mayoba (31) anaefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Jamhuri Manispaa ya Lindi ambaye amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo 
Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.
  Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndg Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie moto huku akijua ni kosa kisheria 
Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo Taarifa zaidi tutawaletea kuhusiana na tukio hilo
Kijana Ismai Mayoba(31)anaefanya kazi Bar ya Mangrove, mkaazi wa Jamhuri, Manispaa ya Lindi, akiwa katika ward namba 6 hospital ya Sokoine -Lindi baada ya kuchomwa moto na vibaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2013

    MUNGU JAMANI HATA SIAMINI MACHO YANGU ! JAMANI WATANZANIA MNAKWENDA WAPI? JAMANI UKATILI UMEKUWA MKUBWA RAIA WANAPIGWA RISASI KAMA WANYAMA PORI NA KUDHULUMU HUKU MABOMU YAKIRINDIMA KAMA SYRIA,SASA KUMUWASHA BINADAMU MWENZAKO MOTO KAMA HUO INA MAANA GANI NDIO MWISHO WA UAMUZI KAMA MTU KASHINDWA MAISHA ? WAHUTUMIWA HAO KAMA WAKISHIKWA IWE MFANO WA KUNYONGWA HADHARANI IWE FUNDISHO.

    HUO NI UNYAMA MKUBWA KWA TAIFA LETU LA TANZANIA MIMI NAISHI GERMANY NA FAMILIA YANGU HUKU WOTE WAMESHTUKA KUONA PICHA HII NA IMEBIDI NIWASIMULIE STORY WAMENAMBIA HAWATAKI KUJA TANZANIA TENA WANAOGOPA NA WAO WASIJE WAKACHOMWA MOTO KAMA HUYO JAMAA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2013

    Tobaa! Jamani hivo vidonda mbona vimeachwa wazi hivo, si atapata infection?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2013

    Huyu ahamishiwe Muhimbili au atakufa. Huko atapata dawa. Haya waafrika kwa waafrika hali kama hii haya akikutwa muhindi au mwarabu itakuwaje. Hii nchi alivyosema Slaa haitakalika ni kweli haitakalika ifikipao 2015 tutafute pa kwenda.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2013

    Duu inasikitisha sana.Wewe uliotoa maoni hapo juu.Hata huko Ujerumani unaweza kuchomwa moto ukiwa mweusi na wabaguzi wa rangi Racists.Huko Ujerumani waafrika wanapigwa visu na kuuliwa ukiwafuniwa na wabaguzi. hivi vitu vinaweza kutokea sehemu yeyote dunia.

    Mtoto wa Kabwela Sweden

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2013

    Poor him, jamani people are so heartless! Ni kwa namna gani unaweza kumuwasha binadamu mwenzio moto kama unawasha gesi upike maharage???? Nashauri atumie asali iliyorinwa kitaalamu inasaidia sana kuponesha vidonda vya moto, nami mwanangu alishawahi kuungua kuanzia kiunoni mpaka kidole gumba cha mguu, asali ilimsaidia sana hata makovu yake hayako stiff, yaani ngozi ipo laini ingawa ina kovu. Pole sana Mungu atakusaidia na haki iweze kutendeka kwa wale waliohusika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...