Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012. 

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012. Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya.

Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo. Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973 wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika mwaka uliotangulia.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Selestine Gesimba
KAIMU KATIBU MKUU

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10/05/2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2013

    Na wale waliojinyna kwa matokeo mabaya itakuwaje? Yaani uholela umejaa katika serikali ya hii nchi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2013

    Wakati NECTA inatumia mfumo mpya lazima(Serikali)mlitaarifiwa mkakubali.Waziri akayasoma.Someone must be responsible kama kweli tunataka nchi iendelee.

    ReplyDelete
  3. SarafinaMay 10, 2013

    Nadhani kuna tatizo kubwa hapa,naona ni kama vile mtu ameenda hospitali akiwa na homa,vipimi vikachukuliwa,wakati majibu yanasubiriwa daktari akaamua kutoa dawa ya ugonjwa tofauti na malaria.Ikiwa tume iliundwa kwa nini tusiambiwe tume imegundua matatizo gani?na kutokana na hayo matatizo ufumbuzi wa kudumu utolewe?Je pengine serikali imeshajua tatizo ila haitaki kusema?(ingawa tatizo linajulikana kwa kila mtu hata kabla tume haijaundwa).Na sasa usahihishaji wa miaka iliyopita na huu wa sasa una tofauti gani ili tujue uliathiri vipi watoto wetu?Ninachoona ni kwamba serikali inatafuta namna ya kuwapoza watu bila kutibu ugonjwa,na ninashawishika kuamini kwamba utratibu wa kusahihisha wa mwaka 2012 ndiou utaratibu sahihi ndio maana umeweza kuweka wazi kiasi cha ubovu wa elimu yetu.Nashauri serikali isitumie njia ya mkato kwa tatizo kubwa kama hili,elimu yetu inashuka kwa kasi hili linajulikana na ufumbuzi wa kudumu nje ya siasa utafutwe

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2013

    Halafu watu wenye "kiherehere" na "kiharusi" cha mawazo wanazema ati bongo kama USA, wanatutupia madongo ya macho siye tuliopo mamtoni turudi bongo.None sense, huu ni upuuzi mtupu, nilivyofanya mtihani wangu wa form four zaidi ya miaka 28 iliyopita niliweka "nadhiri", nisipofaulu na kwenda form six basi, nitazamia meli. I got division ONE nikaenda A level etc, niki mamtoni nafanya kazi ya Profession yangu, sasa wale vijana wa form four ambao hawakuweza kuhimili the frustration and humiliation of FAILURE, wakajinyonga (one in Tabora did just that), au wakajiingiza kwenye umalaya, ufisadi, au due to frustration and possibly undiagnosed and consequently untreated DEPRESSION are now drug addicts or alcoholics, what plans has the govt got to make sure that they are treated fairly (or their families for those whom,the shock of the results were too painful to bear and decided to take gtheir own lives).
    Watoto wa form four, poleni saaana, Mungu awatangulie na awepe nguvu, mliofaulu kihalali muweze kufakikisha na kusomea fani mnazozitaka,na hatimaye msepe kama mjomba wenu mimi Dr Gangwe Bitozi, daktari wa binadamu mamtoni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2013

    Nakubaliana na kila maoni hapo juu, ukisikia serikali zisizojali basi ya kwetu inaongoza.. tatizo kubwa hatutaki kukaa chini na kufikiria.. Anon wa pili umesema exactly nilichokuwa nafikiria kwamba NECTA walivyobadilisha utaratibu lazima wizara iliidhinisha. Arafu leo wanasema 'serikali' imeamulu turudi kule kule kwenye low standards ili tusiudhi watu... Think think think

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...