Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
 Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
 JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew, Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete  kwa marais na viongozi mbalimbali waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2013

    Nimefurahi sana kumuona Mfalme Mswati amevaa suti na tai kwani amependeza sana. Mama Yetu Salma kikwete amependaza sana. Heshima kwa wakuu woote. Salute,

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2013

    hapo mheshimiwa jk anamtania mfalme mswati anamwambia kumbe ukivaa suti unabadilika sana hahahaha hahah hahaha lakini hongera nalipenda sana vazi lako la kiswati teh teh teh

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2013

    Hehehehe Nakubaliana na nyie woote, Mfalme Mswati amependeza sana hakika, amebadilika ghafla alipovaa suti na tai. I like it a lot.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2013

    mfalme mswati mbwembwe tu, suti ndizo zinamfaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...