Ulinzi mkali ambao tayari upo na utazidi kuonekana wakati wa Ujio wa Rais wa Marekani umewafanya baadhi ya Watanzania kujihisi wanadunishwa au kuabishwa. Wapo wengine ambao wanaona kuwa hatua mbalimbali za kiusalama zinazochukuliwa kumlinda Obama, Familia yake na ujumbe wake zinaonesha dharau na kutoaminiwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Wengine wanafika mahali pa kuhisi kuwa Wamarekani wanatudharau sana kiasi kwamba wanatuchagulia nani aonene na Obama (rejea taarifa kwenye gazeti la Mwananchi la leo). Watanzania hawapaswi kujisikia hivyo hata kidogo.
Ulinzi wa Obama ni Mkali iwe ndani ya Marekani au Nje
Wakati wowote Rais wa Marekani anaposafiri iwe ndani ya Marekani au nje ya Marekani ulinzi wake ni mkali na karibu kamili (almost absolute). Kuanzia angalia ambalo anakuwepo (linakuwa no fly zone) na kuwa anaenda na kila kitu kinachoweza kutumika wakati wowote wa dharura yoyote inayoweza kufikirika kutokea. Kuanzia majanga ya moto, maji, maandamano ya kisiasa au hata mapinduzi ya kijeshi ulinzi wa Rais wa Marekani umejiandaa.
Mfano mzuri ni kuwa ikulu ya Rais pale DC – Jumba Jeupe – juu kabisa kuna mzinga wa kutungua ndege – surface to air battery. Lakini kubwa zaidi ni kuwa anga lote linalozunguka Ikulu hiyo ni eneo ambalo ndege haziruhusiwi kuruka (prohibited airspace). Na wakati wowote Rais anaposafiri mahali popote ndege haziruhusiwi kuruka juu yake. Anapotua kwenye uwanja kwa mfano hapa Detroit, hakuna ndege nyingine itakuwa inatua wakati huo huo! Sasa kama hili linatokea Marekani kwa kiasi gani linaweza kutokea Tanzania?
Ripoti hii maalum basi ina lengo la kuwasaidia Watanzania kutokwazika na kiasi cha ulinzi ambao Obama anakuja nao pamoja na usumbufu unaotokana na hilo. Kama msafara wa Rais Kikwete huwa unazusha usumbufu kwa watu basi wa Obama utasababisha kadhia – chukua msafara wa Kikwete zidisha mara 1000!
TEMBELEA LIBENEKE LA MWANAKIJIJI KWA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2013

    Wanatafuta maadui dunia nzima sasa wanapata tabu ya ulinzi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 30, 2013

      Umeliona hilo

      Delete
    2. AnonymousJune 30, 2013

      Wamarekani wameshangazwa kuona wa south Afrika wanavyo protest Obama .Huku USA ukiwa black unatakiwa kumsifiaa tuu lasivyo uta itwa uncle Tom .Wamesifia waafrica

      Delete
  2. AnonymousJune 30, 2013

    ukijijengea maadui duniani basi utakuwa na shida kubwa ya ukosaji amani wa maisha yako na watu wako

    hayo yote yamesababishwa na wamarekani wenyewe kujijengea maadui dunia nzima kwa kutokana na siasa zao mbaya za unyanyasaji na uonevu unaokithiri duniani kote

    kuna msemo wa kimatumbi unaosema UTAVUNA ULICHOKIPANDA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2013

    SURE WA KWANZA HAPO JUU

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2013

    sio mbaya jujiwekea ulinzi,kusafisha mji watanganyika walikuwa wafanye sio kwa kuja obama tu bali iwe ni kazi ya kuendelea

    kitu kibaya nani aonane na obama kwa viongozi wa tanzania hili ni la watanzania wenyewe ndio waliratib na kutowa taarifa kwa vyombo vya ulinzi vya tanzania kushirikiana na cia na fbi

    kauli ya membe ya kuwataka watu wasije mjini wakati obama akiwa nchini hii ni kauli ya kipuuzi watu wamo ndani ya nchi yao wanajihangaikia kutafuta chakula namahitaji yao vipi utawazuwia

    ReplyDelete
  5. sikubaliani nayo kwa mfano:
    Pato letu linategemea pia utalii na kodi ya mapato
    Mfano Uwanja wa Ndege sasa ndege zote Tanzania ziahirishwe kwa muda wa siku moja viwanja vyote si JUlius tu bali na Kilimanjaro Tuanze kwenye mapato:
    kiasi gani tunakosa (tuseme watatulipa marekani ni sawa ) je wafanya biashara zao mfano wenye Appointment zao muhimu au wenye kucatch ndege nyengine kwenda seehemu nyengine kuna wenye ddharura vifo wanataka wawahi hao itakuaje?

    Jengine sijaona Rais wa Marekani kuja Tanzania kisha vyombo vyote vya ulinzi wakaachiwa wao na sehemu nyeti mfano Airport mapinduzi hufanyika watu huwahi sehemu hizo kwanza sasa maofisa wetu wote wamewekwa upande na Airport yetu tumekabidhi watu weupe.

    Huko Marekani kivyaoo kama ndege hazitui akiruka lakini hapa ni kwetu sisi tukienda kwao tunanyanyaswa sasa dharau na manyanyaso haya ndani ya nchi yetu sisi anatusaidia nini wakati ashasema bila ndoa za mashoga misaada hamna? Huu ni unafik ndio maana Zanzibar wanataka mamlaka kamili

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2013

    Nilibahatika kuona msafara wa Bush akiwa Houston, Texas. Yaani ni balaa. Barabara zote zinafungwa. Hizo barabara wanaziita free way. Ni kubwa sana(kama njia kumi hivi) ila zinafungwa huwezi kuamini. Afu kitendo hicho kinafanyika haraka sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 30, 2013

      Bush alikuja Tanza security sio hivyo obama anapenda makubwa mnoo.na atakuwa na butwaa kuona South Africa wanapinga ujio wake .Will Obama ever live with out fame maana fame is more important than his job .

      Delete
  7. AnonymousJune 30, 2013

    Kwa niaba ya Watanzania wenzangu. Issue ya Ulinzi kwa Obama na Team yake inaeleweka, na watanzania hatuna tatizo na taratibu(Protocols) za ulinzi na usala kwa Obama na familia yake. Ulinzi ufanywe na Obama na Team yake aondoke hapa Tanzania akiwa Salama salimini kitu ambacho pia ni Heshima na mafanikio kwa Taifa letu. Ila sasa hizo taratibu z kiusalama isiwe maumivu na minyanyaso ya watanzania na kudhalilishana kwa sababu tu ni moja ya nchi za dunia ya Tatu . Maana sidhani kama minyanyaso na kudhalilishwa kwa raia kunakuwepo pale Obama na Team yake anapotembelea Nchi nyingine zilizokwisha endelea" Dunia ya Kwanza".Mfano Uingereza. Obama anakwenda na uingereza na maisha ya raia yanaendelea kama kawaida hutosikia barabara zinafungwa au watu wanakosa pumzi kwa muda la!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 30, 2013

    Huyo mtu wao kwanini wasimrushe kwa helkopta tu watu watumie njia zao kama kaaaida

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2013

    Halafu mbona huyo obama hana umuhimu huo mbona bush na clinton walikuja zanzibar walitembea kwa miguu mtaani na walifika mpaka kwenye maskan za cuf na wakati huo cuf wakisifika kwa ugaidi kulliko hiyo chadema ya sasa huko bara

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 30, 2013

    Wadau wapendwa mie nimesoma comments zenu woote na nimeelewa kabisa, ila mie naona kutokana na hali ya utata iliyojitokeza Tanzania miezi michache nyuma ni lazima ulinzi wa kiongozi mkubwa kama Obama uhimarishwe ipasavyo, Bobu lilorushwa kanisani Arusha, Bomu lililorushwa kwenye kongamano la Chadema pia. Haya yoote yanaleta utata wa usalama wa Rais wa nchi kubwa kama America. Nilazima wajipange ipasavyo amasivyo wakicheka na kima watavuna mabua hakika. Mie sioni kama ni dharau au ulinzi wao unatudhalilisha kwa namna yoyote ile kabisa kwasababu, ulinzi wanakuja nao wao, ndege ni zao si zetu hapa nchini, magari wanakuja nayo pia wenyewe na tukiangalia hakika jiji letu la Dar limesuguliwa ipasavyo, lina ng'aa sana na linapendeza. WAHENGA WALISEMA "MGENI AJEE MWENYEJI APONE"

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 01, 2013

      Ni kweli kabisa mkae mkijua kuwa chochote kinachotokea Tanzania kipo kwenye ubalozi wao. Tanzania si nchi ya amani tena kama ilivyokua ikijulikana especially kwa hao wamarekani. Kumbukeni kisa cha yule mtoto aliyejaribu kuulipua ubalozi wao mwaka2010 pale Msasani. Kifo cha Mwangosi, Padri Mushi Zenj, mabomu ya Arusha. Unadhani ni Obama anapenda umaarufu au kuna viashiria vya hatari?

      Delete
  11. AnonymousJune 30, 2013

    Obama akiingia nchi yoyote ulinzi wake unakuwaga ni noma. Berlin barabara zilifungwa na wajerumani walibidi wavumilie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...