Mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TSCP), ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) ambao ulizinduliwa rasmi 2010, umedhihirisha jinsi ulivyoshamiri kwa kiwango kikubwa. Mabadiliko makubwa yameshaanza kuonekana katika Miji 7 ambamo Mradi huu unaendelea na shughuli zake. Mikoa hii ni; Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Mbeya, Tanga na Kigoma Haya yalibainishwa hivi karibuni wakati wa Kikao cha kutathimini utekelezaji wa Tscp kilichofanyika Dodoma Hoteli – Dodoma. Kikao hicho kilikusanya wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na wawakilishi wa Halmashauri kwa kusudi la kutathimini kama Mradi huo unaendelea vyema kufanya ipaswavyo au la. Pia kubaini kama matakwa ya mipango ya Mradi yanafanikiwa na kutoa ushauri ambao utasaidia kufanikisha mafanikio ya kutimiza makusudi ya Mradi kama inavyotarajiwa.
wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na wawakilishi wa Halmashauri wakiwa katika mazungumzo juu ya mradi huo.
UJENZI WA STANDI YA MABASI MAKUBWA DODOMAUKIENDELEA, UJENZI HUU UNAOFANYWA NA MRADI WA UENDELEZAJI MIJI WA TSCP, ULIO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2013

    Mikoa saba(7) inawakilishwa na picha mbili zenye mashine moja na wafanyakazi sio zaidi ya ishirini?NIKWELI HUWEZI KUWEKA PICHA ZOTE KATIKA GLOB MOJA. TOA LINK YA WEBSITE TUONE HAYO MAENDELEO.Tafadhalini MEDIA tupeni habari zinazokamilika.jaribuni kuwa bana watoaji taarifa waweze kuwa wawazi.WAAMBIENI WADAU WENU WA BLOG HAWARIZIKI NA HABARI PUNGUFU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2013

    Hiyo ni miradi midogo haifai kufadhiliwa na World bank, au nchi wahisani. Nchi yenyewe inaweza kufanya hivyo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2013

    mbuga za wanyama tunazo,madini tunayo,gesi ipo,bandari tunayo,madini kemkem,haya ni maeneo ambayo tunaweza pata pesa za kutosha kijisaidia ktk miradi midogo midogo ya ujenzi wa taifa letu.
    Inakuwaje tunaendelea kukopa kwa wafadhili kwa miradi midogo?
    Ama kweli kwenye miti hakuna.......

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2013

    Hapana, tunapenda wenyewe umatonya, aghalab utaona kwenye runinga watu na afya zao wamevaa nadhifu wanadai eti shule haina choo, serikali ikawachimbie choo! cha shimo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...