Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba katika Sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Nchini (hawapo pichani) ambao wanastaafu kwa mujibu wa Sheria. Sherehe hizo zimefanyika katika Viwanja vya Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(Katikati)akikabidhi Zawadi ya Kipozea Joto(Refrigerator) kwa Naibu Kamishna wa Magereza, Green Mwaibako(Aliyepo kushoto kwa Kamishna Jenerali) ambaye anatarajia kustaafu rasmi Utumishi wake katika Jeshi la Magereza tarehe 01 Julai, 2013 ambapo amelitumikia Jeshi la Magereza kwa muda wa Miaka 38.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimpongeza Afisa Mteule Daraja la Kwanza wa Jeshi la Magereza, Athumani Chipanje ambaye amestaafu Utumishi wake Ndani ya Jeshi la Magereza na Kituo chake cha Kazi kilikuwa ni Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Makamanda wa Jeshi la Magereza wakifungua Shapeni katika Sherehe za Kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza ambao wanastaafu Utumishi wao uliotukuka Ndani ya Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Sherehe hizo zimefanyikia katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Makamanda wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni Waalikwa ambao walihudhuria Sherehe za kuwaaga Sastaafu wakiburudika na Vinywaji mbalimbali kama inavyoonekana hapo katika Sherehe iliyofana sana ya Kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza ambao Wanastaafu kwa mujibu wa Sheria baada ya Utumishi wao uliotukuka Ndani ya Jeshi la Magereza Nchini(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...