meno ya tembo na Mtambo wa kuteketeza meno hayo. Leo hii Serikali ya Ubelgiji imeteketeza meno ya tembo tani 1.5 iliyoyakamata yakiingingizwa Ubelgiji. Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala  ameipongeza Serikali ya Ubelgiji kwa hatua hiyo na ameziomba nchi nyingine zenye soko la meno hayo kuchukua hatua kama ilivyofanya Serikali ya Ubelgiji. Aidha, Balozi Kamala ameziomba nchi zilizoendelea kusaidiana na nchi zinazoendelea kupambana na ujangiri.
Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji Mhe. Onkelinx akihutubia Wadau wa kupambana na biashara ya meno ya tembo na kuzindua uteketezaji wa tani 1.5 za meno ya tembo. Meno hayo yamekamatwa Ubelgiji katika jitihada za Ubelgiji kupambana na biashara ya meno ya tembo.
Balozi wa Tanzania Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameipongeza Serikali ya Ubelgiji kwa hatua hiyo na ameziomba nchi za Ulaya kushirikiana na nchi zenye mbuga za wanyama  kupambana na ujangiri na kulinda tembo na wanyama wengine.
Aidha, Balozi Kamala alisema  fedha wanazolipa watalii wanapotembelea mbuga za wanyama ni kidogo na haziwezeshi nchi zenye mbuga za wanyama kupambana kikamilifu na majangiri wanaohatarisha tembo na wanyama wengine.
Mtaalamu wa kuteketeza meno ya tembo akipokea meno hayo kuyaweka kwenye mtambo wa kuyateketeza. Ubelgiji leo imeteketeza tani 1.5 za meno ya tembo yaliyokamatwa yakiingingizwa nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...