Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa chakula cha jioni cha kampeni za kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi kampeni ya kadi nyekundu katika kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee katika Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Dkt Augustine Mahiga wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014 kwa ajili ya kuhamasisha mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto hapa nchini.
Mtoto Hamadi Hatibu, 13, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Sahare katika Manispaa ya Tanga akitoa ushuhuda wake jinsi alivyoishi kwa kuvua samaki katika umri wake mdogo.
Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pole sana mtoto Hamad Hatibu, kwa kweli inatilisha imani na kusikitisha sana, khasa kwa huo umri ulionao sasa na darasa ulilopo ni vitu viwili tofauti, ila hulaumini wewe binafsi, hiyo imesababishwa na ugumu wa maisha uliopitia pasina kuwa na msaada wa aina yeyote ile na kupelekea kujishughulisha kimaisha katika umri mdogo kama ulivyotowa ushuhuda wako, hali iliyokupelekea kutoanza shule katika umri muafaka uliostahili. Hata hivyo hujachelewa na elimu haina mwisho, jitahidi kielimu na naamini jitihada zako za dhati katika masomo, ndio zitakazokufanikisha na kukuinuwa zaidi katika maisha yako. Mungu akusaidie In Sha Allah na kukuongoza pema unapostahili.

    ReplyDelete
  2. Yaani ana miaka 13 na yupo darasa la pili? Atamaliza darasa la saba na miaka 19. Ila komaa dogo elimu haina mweisho na Elimu ni funguo wa Maisha bora.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...