Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.
Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-

ELIMU:-
·        Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
·        PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
·        MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
·        BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994

UZOEFU WA KAZI:-

·        Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
·        2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
·        2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
·        1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
·        1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.

Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.

Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.

            Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

18 Desemba, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Congratulation Mr Mataragio. Take your time, but in a year or two make sure you have formed an effective team Working for you. Look all over the world and set up an effective team.

    ReplyDelete
  2. Hongera ndugu Mataragio kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo.
    Tunakukaribisha kwa moyo na ni MATARAJIO yetu utaleta changamoto tosha katika kuongoza taasisi hii ingawaje kwenye uzoefu sijaona uzoefu katika uongozi (upper management). Kila la heri!

    ReplyDelete
  3. excellent decision, tunahitaji diaspora wengi zaidi kwenye hizi nafasi waje nyumbani tuanye kazi pamoja tubadilishe na mind set zetu zielekee kubadilisha taifa na rasilmali zilizopo nchi ikimbie kwenye maendeleo zaidi

    ReplyDelete
  4. Chapa kazi kwa uminifu kadri viongozi wetu wa nchi walivyokuamini mimi binafsi nakuombea mafanikio mema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...