Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Kulingana
na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe
15 Desemba, 2014.
Dkt.
James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi
na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior
Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni
kama ifuatavyo:-
ELIMU:-
·
Masters in Business Development (MBA),
Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
·
PhD (Geochemistry, Mineralogy,
Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla,
Missouri, Marekani (2005)
·
MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo
Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
·
BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, 1994
UZOEFU
WA KAZI:-
·
Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior
Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
·
2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo
Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
·
2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
·
1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold
(Buzwagi)
·
1994 – 1999 -, Exploration Geologist,
Anglo America Corporation.
Miongoni mwa
makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba
ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow;
Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na
Vale Rio Doce.
Aidha, Dkt.
James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi
asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu
sekta hiyo bila malipo.
Kwa
kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa
kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa
katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia
kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18
Desemba, 2014
Congratulation Mr Mataragio. Take your time, but in a year or two make sure you have formed an effective team Working for you. Look all over the world and set up an effective team.
ReplyDeleteHongera ndugu Mataragio kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo.
ReplyDeleteTunakukaribisha kwa moyo na ni MATARAJIO yetu utaleta changamoto tosha katika kuongoza taasisi hii ingawaje kwenye uzoefu sijaona uzoefu katika uongozi (upper management). Kila la heri!
excellent decision, tunahitaji diaspora wengi zaidi kwenye hizi nafasi waje nyumbani tuanye kazi pamoja tubadilishe na mind set zetu zielekee kubadilisha taifa na rasilmali zilizopo nchi ikimbie kwenye maendeleo zaidi
ReplyDeleteChapa kazi kwa uminifu kadri viongozi wetu wa nchi walivyokuamini mimi binafsi nakuombea mafanikio mema.
ReplyDelete