Katika jitihada za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuboresha huduma kwa wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja, leo Shirika la Nyumba la Taifa linazindua huduma mbili, ambazo ni kituo cha huduma kwa wateja na pili ni mfumo wa kulipa kodi za nyumba kwa kutumia simu ya kiganjani. 

Kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kitatumika kuhudumia wateja wetu wote kwa kupiga simu pale wanapohitaji kufahamu juu ya huduma zetu na bidhaa mbalimbali pamoja na kutoa taarifa mbalimbali za shirika zinazohusu huduma kwenye makazi yao. 

Wateja wataweza kupata huduma hii kupitia nambari +255 784 105 200 na + 255 222 162 800. Kupitia kituo hiki Shirika linawaahidi kwamba maulizo na taarifa zozote zitakazoripotiwa zitapewa kipaumbele kwa kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Katika kuendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi kutoka kwa wapangaji wetu, Shirika limeanzisha mfumo wa kulipa kodi kupitia simu za kiganjani ili wapangaji waweze kufanya malipo ya kodi zao bila ya usumbufu wowote kupitia tigopesa, mpesa na airtel money. 

Kupitia mfumo huu, wapangaji wataweza kufanya malipo kwa kutumia simu zao na wataweza kuhamisha fedha kutoka kwenye benki akaunti zao na kwenda Shirika la Nyumba mahali popote walipo na kwa muda wowote ambao ni muafaka kwao bila ya kufika katika vituo vyetu vya makusanyo ya kodi.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...