Balozi wa Simba Octa Mshiu akipokea Hati ya Ubalozi kutoka kwa Rais wa Simba Evans Aveva. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Imani Kajula  

Dhima yetu ya kuendeleza mabadiliko  ndani  ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika  kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali  wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo vya  mapato.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Katika kukuza wigo wake wa kuwashirikisha wapenzi wake katika kuleta maendeleo ya klabu Simba Sports Club inazindua makakati wa kuwashirikisha wapenzi wenye nia ya kuwa chachu ya maendeleo kwenye klabu yao. Simba ni klabu ya wanachama na wapenzi wa Simba, hili  ndilo jambo la msingi
na kujivunia  zaidi. 

Kwa msingi huu wigo wetu wa wapenzi nimtaji muhimu katika kuetekelezamalengo mbalimbali  ya klabu ya Simba. Hivyo basi leo hii klabu ya Simba inazindua rasmi  Mabalozi wa Simba, hawa  ni  wapenzi  wa Simba ambao wako tayari kushirikiana na klabu katika kuleta maendeleo ya  klabu  yetu’’.Aveva aliendelea kusema ‘’ Katika ahadi zetu wakati wa uchaguzi tuliahidi kuwa tumenuia kwa dhati kuleta mapinduzi  ya kimaendeleo  ndani ya Simba. 

Napenda kusema safari yakuendelea  kuifanya Simba kuwa klabu bora ndani na nje ya uwanja imepamba moto. Kwa uhakika malengo mengii kiwemo la kujenga uwanja na kambi ya mazoezi ya Simba sio ndoto. Kupitia  mabalozi  wa Simba na mikakati yetu mingine ya utunishaji wa mapato tunaamini kwa dhati malengo yetu tutayafikia.

Kihistoria Simba imekua ni timu yenye kutendana kufikiriki maendeleo na kutumia nguvu za wapenzi na wanachama, tulianza kwa kuwawa kwanza kujenga jengo la klabu, Mzee Dalali aliona mbali na kununua uwanja Bunju, nasisi  tutaanza ujenzi, hii ndio dhima ya uongozi  ndani ya Simba kupokezana vijiti vya maendeleo’’.
Kwa upande wake MkurugenziMtendajiwa EAG Group LTD ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati ya biashara na masoko wa Simba ImaniKajula  alisema ‘’Zoezi la kuteua mabalozi wa Simba ni endelevu na litafika kila kona ya Tanzania. Hawa ni mashabiki ambao  mawazo, michango yao ya hali na  mali, kutumia ushawishi wao kutaleta maendeleo kwenye klabu yetu. Hawa watakuwa mstari wa mbele kwenye Simba Week kuhamasisha ufanyaji kazi za jamii na kushiriki kwa wapenzi na wapenda maendeleo katika kusukuma  maendeleo ya Simba.
Napenda kuwashukuru  sana Mabalozi hawa kwa kutenga muda na kuwa tayari kusaidia juhudi za kuiletea Simba maendeleo. Uongozi wangu utakuwa bega kwa bega nanyi katika kazi hii adhimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...