Mwakilishi wa Kampuni ya Uchimbaji wa Visima ya
ZENTAS kutoka Uturuki nchini Tanzania Dkt, Mohammed Akbar Akitoa taarifa
za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima chenye urefu wa mita 541
eneo la Mkwalia, Mkuranga, Pwani leo.Kisima hicho kinauwezo wa kuzalisha
maji lita milioni 1.8 kwa siku.
Maji kutoka katika kisima hicho yakitiririka kufuatia kufanyika kwa majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini.
Mtaalam wa mitambo wa
Kampuni ya ZENTAS Sahtn Topal ( katikati) akifafanua teknolojia na vifaa
vilivyotumika kuchimba kisima hicho.Picha na Aron Msigwa/ MAELEZO.
Na.Aron Msigwa- MAELEZO
Wananchi
wa wilaya ya Mkuranga,mkoa wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi
mkubwa wa usambazaji wa maji kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji
wa kisima cha maji chenye urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa
kuzalisha lita milioni 1.8 kwa siku.
Akitoa
taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho mwakilishi
wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS kutoka Uturuki nchini Tanzania
Dkt.Mohammed Akbar amesema wao kama wataalam wanaendelea na majaribio ya
kuyatoa maji kutoka ardhini jambo ambalo limeonyesha mafanikio
makubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...