Na Bashir Yakub.

Mara kadhaa linapoibuka suala la kugawana mali pale ndoa inapohesabika kushindikana masuala kadhaa ya msingi na yanayohitaji uelewa huwa yanaibuka.

Moja ya suala kati ya masuala ambayo huibuka ni hili la kutenganisha na kufafanua hadhi ya mali za wanandoa ili mgawanyo uweze kufanyika kwa haki. Yawezekana mwanandoa akadhani ana haki katika mali fulani lakini kumbe kisheria hana haki hiyo ni mtazamo wake ndio unamsukuma kuamini hivyo.

Halikadhalika yawezekana mwanandoa kudhani hana haki katika mali fulani kumbe anayo haki. Ili kujua una haki ipi katika mali ipi na huna haki katika mali ipi yahitajika kujua misingi ya kisheria inayotumika kugawanya mali za wanandoa.

1.KUGAWANA MALI ZA WANANDOA.

Ieleweke kuwa tunapoongelea wanandoa kugawana mali tunaongelea talaka. Hakuna kugawana mali bila talaka. Na kisheria talaka inapotoka tu swali linalofuata ni habari ya mali na watoto kama wapo. Mali si lazima magari na manyumba lakini pia hata vyombo vya ndani vikiwemo vitanda, makabati, sahani n,k nazo ni mali kwa mujibu wa sheria. Navyo huhitaji mgao.

2. JE KUGAWANA MALI NI NUSU KWA NUSU ?.

Linapokuja suala la kugawana mali wengi hudhani mtindo unaotumika kugawa ni ule wa nusu kwa nusu. Jambo hili si kweli kwakuwa sheria ya ndoa 1971 iliyofanyiwa marekebisho 2002 haisemi kuwa utaratibu wa kugawana mali ni nusu kwa nusu. Sheria hii imeweka msingi mkuu wa kugawana mali ambao ndio hutumika katika mahakama zetu katika kutoa maagizo ya kugawa mali za wanandoa.

Msingi uliowekwa na sheria ni msingi wa kiwango cha mchango wa mwanandoa katika kupatikana kwa mali husika. Kiwango alichochangia mwanandoa katika kupatikana kwa mali hiyo ndicho kitakachokadiriwa na kiwango hicho ndicho atakachopewa.

Kwa hiyo kama ni nyumba ya vyumba sita mmoja anaweza kupata chumba kimoja na mwingine akapata vitano kutegemea na mchango wake. Na mchango hapa sio leta ni lete. Mchango sio hela tu hata kazi za nyumbani anazofanya mama wa nyumbani ambaye haleti hela nazo huitwa mchango ambapo hukadiriwa na kupata kile anachostahili.

3. MALI KABLA YA NDOA NA BAADA YA NDOA.

Katika kutenganisha mali za wanandoa huwa zinatenganishwa katika makundi makuu matatu. Kwanza kuna mali ambazo mtu alikuwa nazo kabla ya ndoa na wakati anaingia katika ndoa ameingia nazo. Kwa mfano mwanamke ameolewa akamkuta mwanaume tayari ana nyumba yake. Pili kuna mali ambazo zimepatikama wakati wawili wakiwa katika ndoa .

Kwa mfano ndoa imefungwa wawili wakaanza kuishi pamoja na taratibu wakaanza kujenga na kukamilisha. Na tatu ni mali ambazo zimepatikana katika ndoa lakini zikiwa hazina uhusiano wowote wa kindoa kwa mfano kurithi au kuzawadiwa mali. Tutaona hapa chini mazingatio ya sheria ya kila moja katika haya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...