"IJUE SHERIA"
Showing posts with label IJUE SHERIA. Show all posts

Na Mwandishi Wetu

Tunaishi katika enzi ambayo skrini zimechukua nafasikubwa katika kila sehemu ya maisha yetu ya kila siku, kuanzia jinsi tunavyofanya kazi na kujifunza, hadinamna tunavyopumzika na kuwasiliana na wapendwawetu. 

Kuanzia tunapofumbua macho asubuhi haditunapolala usiku, wengi wetu hujikuta tumeshikamanana simu janja, kompyuta, na kompyuta mpakato. Uwepo huu wa kudumu wa kidijitali umekuwa wakawaida kiasi kwamba ni rahisi kusahau athari zakekatika ustawi wetu kwa ujumla.

Hayo yanaelezwa na Shaban Salehe ambaye ni Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Jubilee Health Insurance  ambapo anafafanua wanapohitimisha Mwezi wa Ustawi wa Afya ya Akili, ni muhimu kusimama na kutafakari kuhusu madhara yakuwa karibu sana na skrini kwa afya yetu ya akili namiili yetu. Utafiti unaoibuka, pamoja na simulizi nyingibinafsi, unaonyesha hali ya kutia wasiwasi. 

Anasema kutumia muda mwingi kwenye skrini kuna husishwa na kuongezeka kwa wasiwasi, kuvurugika kwa usingizi, uchovu, na hata dalili za kimwili kama vile maumivu yakichwa na macho kuchoka.

Anaongeza kuwa Kundi moja linaloathirika sana na mabadiliko haya ni vijana. Ukuaji wao wa kihisia na kisaikolojia badounaendelea, jambo linalowafanya kuwa rahisikuathiriwa na mazingira ya kidijitali. 

“Mitandao ya kijamii, ingawa huleta fursa ya kuunganishwa, mara nyingi huonyesha maisha yaliyochujwa na kupambwakupita kiasi. Hali hii ya uhalisia wa bandia huwezakudhoofisha hali ya kujiamini, na kuchochea hisia za kutotosha, upweke, na kujilinganisha na wengine. Shinikizo la kufikia viwango visivyo halisi linawezakuwafanya vijana wahisi kuchanganyikiwa na kupotezauhusiano wao halisi na nafsi zao.

“Wakati huo huo, wataalamu wa kazi nao wana kumbwana changamoto zao katika enzi hii ya kidijitali. Matarajio ya kuwa "muda wote mtandaoni" yamefutampaka kati ya kazi na maisha binafsi. Barua pepe, ujumbe, na arifa huendelea kuingia bila kikomo, nakujenga mazingira ambapo ufanisi na kuchokahuambatana kwa hatari. 

“Kutofautisha kati ya muda wakazi na kupumzika kunazidi kuwa kigumu, na hali hiihusababisha msongo wa mawazo wa kudumu nakuchoka kupita kiasi.

“Kukabiliana na changamoto hizi hakumaanishi kuachateknolojia kabisa. Badala yake, kunahitaji mabadiliko yakimakusudi katika namna tunavyohusiana na vifaa vyakidijitali—jambo ambalo mara nyingi hufahamika kama“detox ya kidijitali.” 

Salehe anasema mbinu hiyo hutuhimiza kuchukua udhibiti kwa kuweka mipaka yenye afya, kupanga mudawa kuwa mbali na skrini kwa makusudi, na kukuzauwezo wa kuwa wapo kweli katika ulimwengu wa nje yamtandao. Ni kuhusu kuchagua lini na jinsi ya kutumiateknolojia, badala ya kuhisi kama sisi ni watumwawake.

“Hapa Jubilee Health Insurance, programu yetu yaMaisha Fiti imeundwa kusaidia watu katika safari hii. Kupitia warsha zinazoongozwa na wataalamu, rasilimalina nyenzo za vitendo, tunawawezesha watu kudhibitimsongo wa kidijitali na kujenga ustahimilivu wa akili. 

“Juhudi hizi huongeza kujitambua na kutoa mikakati yakusawazisha mahitaji ya maisha ya kisasa na umuhimuwa kupumzika na kuungana tena na nafsi.Ustawi wa afya ya akili ni sehemu muhimu ya afya kwaujumla. Kutambua hili, Jubilee Health Insuranceinatoa bima pana ya afya ya akili, ikiwa ni pamoja nahuduma za tiba ya kisaikolojia, ushauri nasaha, nahuduma nyingine za msaada. 

“Tunaamini kuwa hudumaza afya ya akili zinapaswa kufikiwa kwa urahisi nazisiwe chanzo cha aibu, ili kusaidia watu kuishi maishayenye uwiano na kuridhika.Katika kipindi hiki cha Mwezi wa Ustawi wa Akili, tunakualika kuchukua muda wa kutafakari kuhusu tabia zako za matumizi ya kidijitali. 

“Fikiria jinsi kuwamtandaoni muda wote kunavyoathiri hisia zako, nguvuzako, na mahusiano yako. Jiulize: Ni lini mara yamwisho ulijitenga kabisa na vifaa vya kidijitali? Ni ninikingeweza kubadilika kama ungepata nafasi zaidi yakuwa na utulivu nje ya mtandao na kujijali?

“Wakati mwingine, uhusiano wa maana zaidi tunaowezakukuza ni ule tulionao sisi wenyewe. Ni katika ukimyausiyo na usumbufu ndipo tunapopata mtazamo mpya, kutunza nguvu ya ndani, na kujenga msingi wa ustawiwa kudumu.

“Tunapohitimisha mwezi huu, tunakuhimiza kujaribumabadiliko rahisi: zima arifa, weka muda maalum wakukaa mbali na skrini kila siku, fanya mazoezi bilakutumia vifaa vya kidijitali, au tumia muda wako katikamazingira ya asili. Hatua ndogo zinaweza kuletamabadiliko makubwa katika kupunguza mzigo wakidijitali na kuongeza uwazi wa akili.”Anasema.

Slashe anaongeza kuwa Jubilee wanajitolea kuwa pamoja nawe katika njia hiikuelekea maisha yenye afya, utulivu, na uwiano bora. Kwa sababu ustawi hauhusiani tu na kutokuwepo kwamagonjwa — bali ni kustawi kimwili, kiakili, na kihisiakila siku.

“Kumbuka, kuishi vyema ni zaidi ya kuhimili enzi yakidijitali. Ni kuimudu kwa njia inayounga mkono afyayako, furaha yako, na uhuru wako.

Tunapohitimisha Mwezi huu wa Ustawi wa Afya ya Akili, tutumie fursa hii kuzima vifaa vyetu vya kidijitali kwamuda ili kupata muunganiko na nasfsi zetu na watu waliotuzunguka.”


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya saruji ya Chalinze Cement, imefungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ili kumtaka Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA), kuirudisha mara moja kampuni hiyo katika daftari la kampuni zilizosajiliwa na kutambulika kisheria nchini.

Kesi hiyo namba 113, ya Mwaka 2023 imefunguliwa leo Mei 15, 2023 na Chalinze Cement kupitia kwa Mkurungenzi Mkuu wake Mohamed Hussein Bahdera.

Aidha kesi hiyo inasimamiwa na Kampuni ya wanasheria nguli kutoka Kampuni ya Mawakili ya Law Associate Co. Ltd.

Katika kesi hiyo, Chalinze Cement imeiomba Mahakama Kuu, kubatilisha haraka amri ya kuifuta Kampuni hiyo pasipo kufuata sheria za makampuni kama sheria inavyotaka.

Itakumbukwa, baada ya vuguvugu la mida mrefu kuhusu madai ya BRELA kuifuta kampuni hiyo, hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara ilithibitisha kufutwa kwa Chalinze Cement, kwa madai nyaraka zake zimegundulika kuwa za uongo wakati wa usajili na Wanahisa wa kampuni hiyo hawatambuliki.

Taarifa hiyo ilitolewa, Machi mwaka huu na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, Bungeni jijini Dodoma, alipokuwa akijibu hoja za wabunge akihitimisha mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Hata hivyo, katika mkutano wa wanahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, Wakili Melchisedeki Lutema, amesema sakata hilo lilianza mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kibiashara ya Septemba 23, 2022 juu ya kuungana au kutokuungana kwa kampuni za saruji ya Twiga na Tanga, yalieleza wazi kuwa yamezuia kuungana kwa makampuni hayo na hayakutoa muda maalumu wa kuisha kwa uamuzi huo.

Aliongeza kuwa, katika mazingira hayo Chalinze Cement walijitokeza kupinga muunganiko huo ili kulinda maslahi ya walaji na mazingira ya usawa wa soko.

Akizungumzia kufutwa kwa kampuni ya Chalinze Sementi, Wakili huyo alieleza wameshangazwa na utaratibu uliotumika kwa kuwa wateja wake hawakupewa taarifa na sababu za kufutwa kwake.

“Chalinze ni kampuni iliyosajiliwa mwaka 2021 na inatambulika na Serikali ndiyo maana hata kwenye rufaa yetu iliunganishwa kwa kuwa Sheria inasema kama yamefanyika maamuzi ambayo mtu anaona kisheria yanaweza kuingilia maslahi yake, anaweza kulalamika...

"Na Chalinze ni mmoja wa watu waliooona maslahi yake yanaweza kuingiliwa ndiyo akalalamika na anaweza kulalamika na haijalishi kama ameanza kuzalisha au au laa," alisema Wakili Lutema


 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAZIRI  Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amewashauri watanzania hususan viongozi mbalimbali, kujenga utaratibu wa kusoma na kuandika vitabu kwa lugha ya Kiswahili ili kuchagiza utekelezaji wa mipango ya taifa, na kubadili fikra za watanzania.

Mhagama ametoa ushauri huo jijini Dar es Salaam wakati wa  uzinduzi wa Maktaba ya UONGOZI na Utambulisho wa toleo la Kiswahili la kitabu cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa cha 'Maisha yangu kusudio langu' kwa lengo la kusaidia watanzania wote wasioelewa lugha ya kingereza kupata fursa ya kukisoma.

Katika uzinduzi wa kitabu hicho pamoja na Maktaba ya Taasisi ya UONGOZI iliyopo Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere wageni waalikwa mbalimbali walihudhuria wakiwemo viongozi walioko kwenye utumishi pamoja na waliostaafu.Pia waliokuwepo wawakilishi wa mataiafa mengine kadhaa.

"Machapisho na vitabu vingi nchini vimeandikwa kwa lugha za kigeni,  hivyo ili kuondoa dhana ya kuwa watanzania kukosa utaratibu wa kusoma vitabu kwa kigezo cha kutoelewa lugha, waandishi wa vitabu wanatakiwa kujikita zaidi kuandika vitabu vyao katika lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia maadili natamduni za Mtanzania.

"Tukiwa na vitabu ambavyo vitaandikwa kwa lugha rafiki naamini wengi watapenda kusoma lakini tusiishie kuandika vitabu vyenye mambo magumu peke yake ,ni vema vikaandikwa na vitabu ambavyo vitafanya msomaji kutoona uvivu kukisoma,kitabu kinaweza kuandikwa katika historia ya kufurahisha na hivyo kuvuta wengi,"amesema Waziri Mhagama.

Aidha Waziri Mhagama ametoa Rai kwa Taasisi ya UONGOZI kuangalia namna ya kuhakikisha vitabu ambavyo ambavyo wanavyo kwenye maktaba yao kikiwemo kitabu cha Hayati Mkapa vikasambazwa kwenye shule za msingi, sekondari pamoja na vyuoni na hiyo itaongeza hamasa ya Watanzania kusoma vitabu.

"Nashauri kwa Taasisi ya UONGOZI hiki kitabu cha mzee wetu Benjamin Mkapa ni vema kikasambaza mashuleni wanafunzi wetu wasome, na wakianza kusoma wakiwa wadogo itafanya wawe na muamko wa kusoma vitabu."

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na  Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya Uongozi, Balozi Ombeni Sefue, ameeleza kwamba viongozi na watanzania kwa ujumla wanapaswa kumtendea haki Hayati Rais Mkapa kwa kusoma kitabu hicho alichokiandika kwa ajili ya ila mtanzania.

Wakati Mbunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam Profesa Kitila Mkumbuko amesema kuna kila sababu ya Serikali kuweka mazingira rafiki wananchi kuibu mijadala na hivyo itasababisha watu kuandika vitabu na kusoma." Kumekuwa na changamoto kwa sasa vijana vyuoni wanaogopa kuweka majukwaa ya majadiliano kwasababu wakionekana wanajadiliana wanaonekana wanafanya makosa.

"Enzi zetu tukio Chuo Kikuu mijadala ilikuwa inafanyika bila vikwazo, na kweye mijadala ndiko ambako watu wanalazimika kusoma vitabu ili kuwa na uelewa mpana wa mambo na kujenga hoja,"amesema na kuongeza kwamba bado kuna changamoto ya watu kupenda kusoma vitabu na matokeo yake hata viongozi wanapokosea hakuna wa kuhoji.

"Napenda sana kusoma vitabu tangu zamani na bahati nzuri nimewahi kuwa Waziri Kuna wakati unazungumza jambo na unapotafakari unaona kabisa sikuwa sahihi lakini hakuna aliyekuwa akihoji, lakini kama kungekuwa na utamaduni wa watu kusoma vitabu wangekuwa na uwezo wa kuhoji.Rai yangu ni lazima tujenge utamaduni wa kupenda kusoma vitabu,"amesema Profesa Mkumbuko.

Kwa upande wa   Mke wa Hayati Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa akizungumza kwenye uzinduzi wa kitabu cha Hayati Mkapa ambacho kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili amesema pamoja na kuzindua kitabu hicho kwa lugha ya Kingereza lakini kiu kubwa ya Mzee ilikuwa ni kuwa na kitabu chenye lugha ya Kiswahili kinachozungumzia maisha yake na sasa  Taasisi ya Uongozi wametimiza hilo.

Zitto Kabwe yeye alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi huo amesema amekuwa na utamaduni wa kupenda kusoma vitabu huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi kuandika vitabu vinavyozungumzia maisha yao pamoja na uzoefu wao kwenye masuala ya uongozi.

"Hiyo itasaidia Watanzania hasa vijana kutambua historia ya maisha ya viongozi akitoa mfano amemfahamu zaidi Benjamin Mkapa kupitia kitabu chake kwani wakati anamaliza uongozi wa nchi yeye( Zitto) ndio alikuwa anamaliza sekondari,"amesema Zitto.

Awali akizungumza kabla ya uzinduzi huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Kadari Singo ameeleza tukio hilo limejumuisha utambulisho wa toleo la Kiswahili la tawasifu ya Rais wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa, “Maisha Yangu, 
Kusudi Langu: Kumbukizi ya Rais wa Tanzania”. 

Amesema awali kitabu hicho kiliandikwa kwa lugha ya Kiingereza na kuzinduliwa Novemba, 2019 na hayati John Pombe Magufuli, Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Wakati wa uzinduzi "Mheshimiwa Rais aliiagiza Taasisi ya UONGOZI itafsiri kitabu hicho kwenda kwenye lugha ya Kiswahili ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

"Washiriki kwenye tukio hili ni pamoja na mke wa Rais Mstaafu Mkapa, Mama Anna Mkapa; 
Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya UONGOZI; viongozi waandamizi kutoka kwenye sekta 
za umma na binafsi; washirika wa maendeleo; na wanachama wa Maktaba hiyo. "

Maktaba ya Uongozi ilianzishwa mnamo mwaka 2012 kwa lengo la kuhamasisha 
utamaduni wa kutoa maarifa na kujisomea nchini na Barani Afrika kwa ujumla na kwamba kupitia Maktaba hiyo, viongozi, watafiti, wanafunzi na jamii kwa ujumla, wanaweza kufikia machapisho ya masuala ya uongozi na maendeleo endelevu yanayoendana na 
mabadiliko mbalimbali duniani. Maktaba ina vitabu na majarida zaidi ya 50,000, ikiwemo 
vile vilivyochapishwa na katika mifumo ya kielektroniki. 
Waziri  Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya UONGOZI  Kadari Singo wakiangalia vitabu vilivyopo kwenye maktaba hiyo.
Waziri  Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akiwa amekata utepe kuashiria kuzindua rasmi Maktaba ya UONGOZI iliyopo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri  Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama(wa nne kulia), Mke wa Hayati Rais Mstaafu Benjamin Mkapa,Mama Anna Mkapa ( wa tatu kushoto) wakiwa na viongozi wengine wakati wa  uzinduzi wa Maktaba ya Uongozi na Utambulisho wa toleo la Kiswahili la kitabu cha  Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa cha 'Maisha yangu kusudio langu' uliofanyika  Jijini Dar es Salaam.
Mkuruenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Bakari Manchumu (katikati) akiongoza mdahalo ulioangazia yali ya usomaji wa vitabu nchini katika hafla hiyo. (wa pili kushoto), ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo, na (wa tatu kulia), ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Siasa cha ACT - Wazalendo Zitto KabweMatukio mbalimbali katika picha wakati wa tukio hilo










 


Imeandikwa na Bashir  Yakub, WAKILI - +255 714 047 241.

Tatizo ni vyuo vya sheria. Tatizo linaanza  na sifa za udahili wa wanafunzi wanaostahili kusomea sheria katika vyuo, na Pili mfumo wa ufundishaji vyuoni.

Kuna vyuo hadi mwenye D flat, D English, D kiswahili na D history anapata na nafasi ya kusoma sheria.
Sasa hivi karibia hamna chuo hakitoi degree ya sheria. Chuo hata kikiwa kipya moja ya kozi ambazo wanaanza nazo na ya sheria lazima iwemo.

Mchanganyiko huu hauwezi  kuwa salama ukifika Law School ambapo maadili na taaluma ya sheria inasimamiwa kwa uthabiti.

Hatusemi vyuo vya sheria visiwe vingi ama watu wasidahiliwe kwa wingi, tunazungumzia ubora wa vyuo hivyo katika kutoa taaluma hiyo, na ubora wa wadahiliwa wenyewe.

Niwaambie kitu, asilimia 90 ya wanafunzi wanaomaliza sheria katika vyuo vyetu hawawezi hata kuandaa kiapo(affidavit). Kiapo tu.

Simsingizii mtu, mahakimu na mawakili mnaokaa na wanafunzi hao wakija field mnajua na mmekuwa mkikilalamika sana kuhusu hili.

Nazungumzia kiapo wala sizungumzii kuandaa mashitaka(Plaint au Charge) au utetezi( Wsd), kiapo tu hawajui.
Mtu kama huyu unataka Law School iseme amefaulu, ili akafanye nini mtaani. Akatoe huduma gani. 
Kuna kitu jamii inapaswa kuelewa. Law School haizalishi tu Mawakili  bali Mahakimu na Majaji. Tokea ilipoanzishwa hawi mtu Hakimu ama Jaji isipokuwa amefaulu Law School.

Unaonaje mtu kama Jaji ama hakimu mwenye mamlaka ya kuhukumu mtu kunyongwa hadi kufa, kuhukumu kifungo cha maisha jela, kifungo cha miaka 30, kuhukumu upoteze nyumba ama mali yako nk awe mtu aliyefaulu kiujanjaujanja tu ilimradi. Haiwezekani

Law School inahiaji watu "Pure" na wala haimuonei yeyote. Inahitaji watu ambao watabeba majukumu mazito kama hayo niliyoainisha hapo juu.  

Hayo majukumu ni mazito sawa na ya udaktari. Ni majukumu ambayo mstari wake ni kati ya kifo na uhai.
Wanafunzi wenyewe wanajua na ndio maana wakifeli wanakimbilia kwenye media. Zipo taratibu za rufaa kwa waliofeli lakin hawataki kuzitumia sababu wanajua hawatatoka kutokana na ukweli. Wanajua kabisa wamefeli kwasababu hawajaiva inavyostahili.

Na suala la kuhakikisha Wakili anaiva vizuri kabla ya kuapishwa halijaanza na Law School. Lilikuwepo hata kipindi cha Bar Exam kabla Law School haijaanzishwa.  Mwendo ulikuwa huu huu. Waulizeni waliopitia mfumo huu wa Bar Exam watakuelezeni. Mtu alikuwa akirudia mitihani hii hata mara 15 ili aweze kufaulu na kuapishwa kuwa Wakili. 

Lengo ni hilohilo kumuandaa mtu sahihi atakayebeba haya majukumu mazito ya kifo na uhai.
Kwa ufupi, kama kuna sehemu ya kushugulikia kuondokana na kadhia hii ni vyuo vya Sheria. Mifumo ibadilike kuanzia sifa za udahili hadi ufundishaji.

Sifa za udahili wa shetia zimeshushwa mno, Pili Wajitoe katika kufundisha Theory na wajikite katika Practical. Law is about practise 80%  and theory 20%.

Tusitafute mchawi Law School. Na ukitaka kujua ukweli wa hili ni nadra mno tena mno mtu ambaye amemaliza chuo akapractise kwa muda aidha kwa mawakili au mahakamani then akaenda Law School, kumkuta amefeli. 

Hao wachache mnaosikia wanafaulu wengi sio fresh from school. Ni watu ambao wametoka ofisi za mawakili  au wamepractise mahakamani.

Hawa wa kutoka chuo moja kwa moja Law School hufeli karibia wote, itokee tu. 
Kwahiyo ni muhimu kuangalia hayo mambo mawili, Kwanza sifa za udahili wa wanafunzi ambao wanatakiwa kusomea sheria, Pili mfumo wa vyuo ubadilike kutoka theory na kuwa practical zaidi.

Tuachane na Law School iandae watu Mahiri. Tunahitaji watu mahiri wabebe majukumu mazito ya kifo na uhai.
 Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Taasisi Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo Machi 10, 2022 Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Machapisho, Law Shool Profesa Zakayo Lukumay akieleza jambo mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene pamoja Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud mara baada ya waziri huyobn kumaliza kufanya ziara kwenye taasisi hiyo leo Machi 10, 2022 Dar es Salaam.
 Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene baada yanm kumaliza kufanya ziara yake kwenye taasisi hiyo leo Machi 10 2022 Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Geofrey Pinda aliyesimama akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheri kwa Vitendo baada ya Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene kumaliza kufanya ziara kwenye Taasisi ya hiyo leo Machi 10, 2022 Dar es Salaam
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akipokelewa na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) Dkt. Benhajj Masoud pamoja na watumishi wa taasisi hiyo kufanya ziara kwenye Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo tarehe Machi 10, 2022 Dar es Salaam.

WAZIRI wa Katiba na Sheria George Simbachawane amevushauri vyuo vinavyofundisha taaluma ya sheria nchini kuhakikisha wanaweka vitengo vya kutoa msaada wa huduma ya kisheria kwa wananchi wote hasa wale wasiokuwa na uwezo ili kupeleka haki mbele
kama ambavyo shule ya sheria nchini inatoa huduma hiyo.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo Machi 10 2022, wakati wa ziara yake katika Chuo cha sheria Dar es Salaam.

Amesema kuwa huduma ya msaada wa sheria ipo kwa mujibu wa sheria na kwamba Serikali imeanzisha kitengo hicho " Ofisini kwetu yupo Mkurugenzi anayeshughulika na huduma na anasajili watoa huduma hiyo na wizara hiyo inahakikisha kila mwananchi anapata haki yake

"Nchi yetu bado inahitaji wanasheria ama mawakili ili kusaidia wananchi na Taifa kwa ujumla na ndio maana hivi karibuni serikali imetunga sheria ya msaada wa kisheria ambao unatolewa bure na Taasisi, watu mbali mbali na wizarani ambako kuna mkurugenzi anayehusika na usajili ya huduma hiyo ya msaada wa kisheria ambae pia anawasajili watoa huduma.

"Nakipongeza Chuo hiki kwa kuwa na utaratibu mzuri kwani nimekuta wamefungua kitengo cha msaada wa kisheria na wanatoa huduma hii bure" amesema Simbachawene.

Amesema, amefurahi sana kuona namna wanafunzi wa Chuo hicho wanavyoandaliwa kwenda kutatua changamoto mbali mbali za kisheria kwa wananchi na Taifa kwa ujumla .

Aidha nakipongeza sana Chuo hiki na uongozi mzima kwa kufanikisha ile kazi ambayo serikali ilikusudia ya kuandaa mawakili ili waweze kuwa na uwezo wa kushindana na mawakili wengine dunia na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

" Saizi dunia inaishi kwenye mitandao katika makubaliano, unapokuwa na wanasheria wazawa ambao wameiva vizuri unakuwa umetengeneza silaha kubwa katika nchi kama vile tunavyoweza kununua silaha za kijeshi katika kulinda nchi", amesema Simbachawene

Aidha Simbachawene amesema, Chuo cha sheria kinaandaa watu kwenda kufanya uwakili na siyo mwanafunzi kufaulu mtihani, kwa hiyo ule uwezo ambao mwanafunzi atakuwa ameupata kuweza kumsaidia mteja wake kwa vitendo ndio utakaomuwezesha kufaulu vizuri.

Amesema, uwakili ni kuongea siyo kuandika hivyo kama wakiingia Chuo wanafunzi mia nane na wakatoka mia mbili sisi tunaamini kuwa Chuo kinafanya kazi nzuri kwa hawa wanasheria wanaotaka hapa wanaenda kusimamia viapo, mikataba kuandaa kuunganisha watu na kusuluhisha mambo mbalimbali.

" Hakuna maneno maneno kwenye taaluma ya sheria kama maeneo mengine, hivyo hatuwezi kuchukua kama mtihani wa shule au vyuo vya kawaida ili wanafunzi watoke tu, hapana ikifanyika hivyo tutakuwa tumearibu maana nzima ya kuwajengea uwezo wanafunzi hawa ili tuweze kuwa na mawakili wazuri katika Kanda na dunia kwa ujumla.

Aidha amesema, Chuo kinahitaji kuwa na vitendea kazi vya kisasa, ili hatimae nao waweze kwenda sambamba na Mhimili wa Mahakama ambao kwa sasa umefika mbali katika masuala ya ICT kwabi sasa unaweza pata huduma za Utabiri kimahakama kutokea mahali popote kwa njia ya mtandao.

Naye, Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud amesema wamefarijika na ziara ya Waziri huyo chuoni hapo kwa kuwa imewaongezea hamasa katika masuala mbalimbali na kwamba wataendelea kutimiza majukumu yao hasa katika kuhakikisha wahitimu wanaotoka mahali hapo wanakuwa na weledi wa kutosha.

Mhe. Dkt Paul F. Kihwelo Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa mafunzo ya haki za watoto  katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Jaji Mohammed Gwae (wapili kulia), Katibu wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Aloyce Musika (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma leo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii wakiwa katika Kikao cha Kamati hiyo, kilichofanyika leo Septemba 10, 2021, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uangalizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Aloyce Musika, ambaye ni Katibu wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Idara ya Huduma za Uangalizi katika Kikao cha Kamati hiyo, kilichoifanyika, jijini Dodoma, leo.Katibu huyo alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2020 hadi kufikia Julai 2021, Idara imefanikiwa kuwasajili Wafungwa 3496 na kuwawezesha kutumikia adhabu nje ya magereza hivyo kupunguza msongamano magerezani.
 

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Jaji Mohammed Gwae, akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii baada ya kutambulishwa kwa Wajumbe kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamati hiyo. Kikao hicho kilifanyika leo Septemba 10, 2021, jijini Dodoma. Mwenyekiti huyo aliwaambia Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni wajibu wao kufuata sheria na kumshauri Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene.

Na Innocent Kansha, Mahakama-Njombe

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi ametoa wito kwa Mahakimu na Wasajili kote nchini kuacha kupokea ama kusajili Mahakamani mashauri yasiyo kuwa na tija ili kupunguza kulundika kesi zisizo na msingi kwa lengo la kuwapunguzia wananchi usumbufu.  

Akizindua rasmi Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ya Njombe mnamo Aprili 27, 2021 Mhe. Dkt. Feleshi alisema kwa kufanya hivyo Mahakama itaendelea kuchochea uchumi na kuleta amani kwa wananchi. 

"Hakimu au Msajili unapoletewa hati ya shauri jipya liwe la Madai au Jinai unatakiwa upokee shauri lenye sifa ya kusikilizwa na kama shauri halikidhi vigezo unatakiwa kutumia amri za awali “Initial Orders” kwa mujibu wa sheria kulimaliza shauri hilo lililopo mbele yako ama kwa kulirudisha likafanyiwe marekebisho au likafanyiwe upelelezi wa kina," alisema Mhe. Jaji Kiongozi.

Aliongeza kwa kusema kuwa kabla ya kutoa amri ya kuita watu Mahakamani, inabidi kujiuliza kama hati  ya madai inaeleweka na kwa upande wa jinai Hakimu ni vyema kutumia sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kuona kama shauri linakidhi vigezo vya kupokelewa na kusajiliwa Mahakamani, hii itasaidia kupunguza mashauri kukaa Mahakamani muda mrefu pasipo kuwa na ulazima bila kusikilizwa.

Jaji Kiongozi alisema ni rai yake kwa Mahakimu kuwa yale mashauri ya jinai yasiyokuwa ya makosa makubwa yanapopokelewa Mahakamani siku hiyo hiyo mshitakiwa asomewe mashitaka na hoja za awali ili kesi ianze kusikilizwa wakati huo huo.

Aidha, Jaji Kiongozi aliongeza kuwa Mahakama kwa sasa itaanza kushughulika na Mahakimu wanaopokea kesi sizio na hadhi ya kupokelewa Mahakamani kwani eneo hili ni moja ya maeneo ya kiukaguzi na kwa kutambua kuwa Mahakama inao wajibu wa kutoa elimu kwa watu wanaoleta kesi za namna hii kwa kutoa ufafanuzi wa kwa nini mashuri ya namna hiyo yasipokelewe Mahakamani kupitia Maafisa Masjala.

Jaji Kiongozi alitumia wasaa huo kutoa ushauri kwa wadau wa Mahakama kuwa kila eneo lenye mamlaka ya kiutawala na idadi kubwa ya watu kwa maana ya makazi mengi kuwe na gereza dogo la Mahabusu ili kuisaidia Mahakama kusogeza huduma za utoaji haki karibu zaidi na wananchi kwani Mahakama kama taasisi tayari inayo miundombinu ya kutosha ya kusaidia kutoa huduma.

"Ikumbukwe kwamba kabla ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe mwaka 2012, kupitia Tangazo la Serikali Na. 9 la tarehe 01/03/2012 wananchi wa hapa Njombe na wilaya zake, ambazo ni Njombe, Ludewa, Makete na Wanging’ombe, walilazimika kusafiri umbali wa kilomita 223 kufuata huduma za Mahakama ngazi ya Mkoa, mkoani Iringa," aliongeza Jaji Kiongozi.

Mhe.Jaji Dkt. Feleshi, aliongeza kuwa umbali huo ulikua mrefu na wananchi waliathirika kwa kutumia muda wao mwingi kutafuta huduma za Mahakama, muda ambao wangeutumia katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii. Lakini pia, umbali huo kwa namna moja au nyingine uliwakatisha tamaa baadhi ya wananchi kufuatilia haki zao Mkoani Iringa na wengine hawakuweza kumudu gharama za kujikimu, hivyo kukosa haki zao.

Wananchi walio wengi katika Mkoa huu ni Wakulima, wafanyabiashara na Wafugaji, jamii ambayo kwa hakika inahitaji muda mwingi ili waweze kujikita katika shughuli zao za kiuchumi. Uwepo wa jengo hili jipya ni nafuu na ukombozi kwa wananchi wote wa Njombe kwani litaokoa muda na fedha ambazo wanachi walikuwa wakipoteza hapo awali, aliongeza Dkt. Feleshi.

Akiendelea kufafanua Jaji Kiongozi alisema moja ya mikakati iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa kila eneo jipya la kiutawala linaloanzishwa, kunajengwa Mahakama, kwa kuwa huduma za Mahakama ni muhimu kama ilivyo huduma nyingine za umma. Serikali inapoanzisha Mkoa, Wilaya, Tarafa na hata Kata mpya ni kwa sababu kwamba wananchi wa maeneo hayo wanahitaji huduma za Serikali kwa ukaribu na wepesi zaidi. Vigezo hivyo vinaonesha pia umuhimu wa kusogezewa kwa huduma za Mahakama karibu na wanachi.

Kwa sasa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe wanasajili wastani wa mashauri 524 kwa mwaka, pia Mkoa huo una mashauri mengi ya mauaji ambayo husikilizwa na Mahakama Kuu. Jengo hili linayo nafasi ya kutosha kuwezesha Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu kuendesha vikao vya Mahakama Kuu bila tatizo lolote.

“Natoa rai kwa watumishi wa Mahakama kwamba, majengo haya ya kisasa na miundombinu bora, iambatane na upatikanaji wa huduma bora kwa mwananchi. Niwasihi watumishi wenzangu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe na Mahakama nyingine hapa nchini kubadili mienendo na tabia ambazo zinakiuka miiko na maadili ya kazi kwa watumishi wa umma”, alisisitiza Dkt. Feleshi.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Eng. Lubilya Marwa akitoa salamu za mkoa aliushukuru Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kukamilisha ujenzi wa miradi mitatu (3) ya majengo ya kisasa ya Mahakama katika Wilaya tatu kati ya nne za Mkoa wa Njombe.

“Uzinduzi wa Mahakama hizi tatu za Njombe, Makete na Wanging’ombe kwetu sisi ni tukio la kihistoria kwa kipindi kirefu Mkoa umekuwa ukifanya kazi zake kwenye mazingira magumu si kwa Mahakama tu hata Taasisi zingine na sasa Muhimili wa Mahakama utafanya kazi katika mazingira bora na rafiki”, alisema Mkuu wa Mkoa Eng. Marwa.

Eng. Marwa aliongeza kuwa ni imani ya Uongozi wa Mkoa kuwa hata Wilaya ya Ludewa iliyosalia na yenye changamoto kubwa itafikiliwa na kutengewa bajeti ili nayo iweze kupata Jengo lake la Mahakama hali itakayo imarisha utendaji wa shughuliza zake za kimahakama.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa Mhe. Pentelni Mlisa Kente alisema Mahakama ya Tanzania imepitia nyakati ngumu na historia ndefu kuhusu suala la majengo nyakati fulani Mahakama ilikuwa ikitoa huduma zake kwa kutumia majengo ya Chama Cha Mapindunzi hadi ilipofika mwaka wa 1992 kulipoanzishwa Vyama Vingi vya Siasa, Mahakama ikanza kusaka hifadhi huku na huku.

“Sisi kama Mahakama leo tunayo furaha sana kupokea jengo hili la kisasa nadhani hata wewe Mkuu wa Mkoa furaha uliyonayo haiwezi kulinganishwa na sisi wanamahakama kwa sababu kuna msemo unasema ‘Huwezi kulia msibani ukamzidi mama wa marehemu”, alisisitiza kwa bashasha Jaji Mfawidhi.

Naye Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Martin Chuma aliwaomba watumishi wa Mahakama na wadau wote watakao tumia jengo hilo la kisasa kufanya kazi kwa bidii na huduma wakazotoa zisawiri muonekeno wa jengo husika, ikiwa ni pamoja na kutenda kazi kwa kuzingatia viapo vyao.


 

Na Mary Gwera, Mahakama

Wadau wa Kamati ya Kitaifa ya Kusukuma Mashauri ya Jinai nchini kila mmoja kwa nafasi yake wametakiwa kusimamia sheria ambazo hazitoi mwanya wa kuwa na mlundikano wa mashauri Mahakamani na msongamano wa mahabusu gerezani.

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo alipokuwa akifungua rasmi kikao chao mwishoni mwa wiki iliyopita, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma alisema kuwa kumekuwa na ucheleweshaji wa upepelezi hali inayosababisha mlundikano wa mashauri na mlundikano wa Mahabusu.

“Bado hatusemwi vizuri kwenye suala la mlundikano wa mashauri unaosababisha msongamano wa mahabusu gerezani kwa sababu mbalimbali kama vile kutokamilika kwa upelelezi kwa wakati, Upatikanaji mashahidi, idadi ndogo ya rasilimali watu kama vile Majaji na Mahakimu,waendesha mashtaka na kadhalika,” alisema Mhe. Chuma.

Alisema kuwa changamoto zilizoainishwa zinaweza kuepukwa iwapo kila mdau atafuata sheria, miongozo na taratibu zilizowekwa ili kuwezesha mchakato wa utoaji haki kufikika kwa wakati na ufanisi.

Msajili Mkuu aliongeza kuwa ili kudhibiti hayo Wadau wote wanatakiwa kuwa na utayari wa kutoa huduma na kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake na kutumia mamlaka tuliyonayo hata pale inabobainika kuwepo mashauri mahakamani yasiyo na tija.

“Kwa mfano kusimamia vifungu vya 91,98,225 vya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai kwa upande wa waendesha mashtaka na Mahakama. Mamlaka ya Mkuu wa Kituo kutoa adhabu ya faini; kwa mujibu wa kifungu 170 (6) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (the Criminal Procedure Act (Cap 20 RE 2019),” alibainisha.

Asisitiza kuwa kwa mashauri yasiyokuwa na ushahidi wa kutosha, yanatakiwa kuwasilishwa maombi maalumu mahakamani ya kuomba amri ya uangalizi kwa mujibu wa vifungu 70-73 vya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (the Criminal Procedure Act (Cap 20 RE 2019).

Kwa upande wa Magereza, Mhe. Chuma alishauri kuwa na  Matumizi ya adhabu mbadala ambapo Afisa Ustawi wa Jamii anawajibika kupendekeza adhabu mbadala kwa watuhumiwa waliotiwa hatiani kwa makosa ambayo adhabu husika ni chini ya miaka 3, kama inavyobainishwa katika kifungu 3 (1) cha Sheria: The Community Services Act (Cap. 291 R.E. 2019).  

“Hivyo, kupitia kikao hiki ni matarajio yangu mtatoa mapendekezo zaidi yatakayowezesha kuendeleza maboresho ya huduma ya utoaji haki nchini ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo iliyopo kikatiba,” alisisitiza.

 Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kusukuma Mashauri ya Jinai nchini yenye Wajumbe kutoa Mahakama, Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Chama cha Mawakili wa kujitegemea Tanganyika (TLS), Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Magereza, TAKUKURU kinalenga kujadili mafanikio na changamoto ya uendeshaji wa mashauri ya jinai na mfumo wa jinai kwa ujumla na kupendekeza namna bora ya kushughulikia mashauri hayo.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kusukuma Mashauri ya Jinai nchini (hawapo pichani) alipokuwa akifungua rasmi kikao cha Kamati hiyo katika Ukumbi wa katika ukumbi wa mafunzo wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto jijini Dar es Salaam, Aprili 23, 2021. Kushoto ni Mhe. Sharmillah Sarwatt, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

Washiriki wa kikao wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.

Mhe. Msajili Mkuu akiwaonyesha Wajumbe kijitabu cha utekelezaji wa Majukumu ya Mahakama kwa mwaka 2020. Ametoa rai kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kukisoma na kujua mafanikio, changamoto na mipango mbalimbali ya Mahakama ya Tanzania.

 Na Jusline Marco-Arusha

Wizara ya Katiba na Sheria imefanikisha maboresho ya mfumo wa haki jinai ambayo yatasaidia kutoa muongozo kwa vyombo vyote vya utoaji haki ili uweze kutoa haki kwa wakati kwa watu wote wakiwemo watoto walio katika upinzani wa sheria na waliokutana na sheria.

Akizungumza katika kikao cha kwanza cha Jukwaa la Haki Mtoto,kikao kilichofanyika jijini Arusha Bi.Emma Pastori Lyimo Mkurugezni wa utawala na rasilimali watu kutoka ofisi na wizara ya katiba na sheria kwa niaba ya mwenyekiti wa Jukwaa hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba ma Sheria Prf.Sifuni Mchome alisema licha ya changamoyo zolizokuwepo katika mkakatibwa awali wa utekelezaji kumekuwapo na mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kutunzwaili kuendelea kulindwa na kuhifadhi haki ya mtoto kwa maendeleo endelevu.

"Sisi sote ni wadau muhimu katika kuhakikisha kuwa masuala ya haki mtoto yanasimamiwabkwa uweledi."Alisema

Alisema ni vyema changamoto zolizopo kutumiwa kama fursa ya za kipanga na kutekeleza zumuni la lengo lolilokusudiwa kwani watoto ndiyo kiini cha taifa lolote na oli taifa liendelee kuwepo ni lazima watoto waweze kuwepo.

Alirleza kuwa Serikali chini ya utaratibu wa ofisi ya waziri mkuu iliandaa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kuanzia ngazi ya taifa hadi kijiji kwa lengo la kuyalinda makundi maalumu ndani ya jamii dhidi ya vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikifanya dhidi yao.

Vilevile aliwataka wajumbe hao kuongeza nguvu na rasilimali nyingi zaidi katika katika kulinda haki za mtoto kwa ajili ya uhai,ustawi,ulinzi na usalama wa tanzania ya leo na hata baadae oli taifa liweze kuwepo.

Aidha aliongeza kuwa katika utekelezaji wa mkakati wa kwanza wa miaka 5 ambao ulikuwa mwaka 2013/2017 ambapo amesema kwa ushirikiano wa pamoja wataweza kuona utekelezaji wa mkakati wa 2021 hadi 2425 wakiuwianisha na mkakati wa awali na malengo yaliyokusudiwa katika makakati wa pili amabayo yataboresha mkakati wa awali kwa ajili ya kumtetea mtoto.

Kwa upande wake wakili wa serikali kutoka ofisi ya Taifa ya mashtaka Beatrece Mpembo kwa niaba ya washiriki wenzake katika kikao hicho aliishukuru wizara ya katiba na sheria kwa kuwaamini na kuweza kuwakutanisha tena kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati wa pili baada ya mkakati wa kwanza kumalizika.

Alisema kuwa mkakati wa pili umetoa dira ya kuonyesha mafanikio ambayo waliyapata kipitia mkakati wa kwanza,na kuwaonyesha mapungufu ambayo waliyapata kupitia utekelezaji wa mkakati wa kwanza ambapo mkakati huo pia unatoa uelekeo wa nini kifanyike na kukamilisha kupitia taasisi husika.

"Kwa niaba ya washiriki wenzangu tunauzoefu na kwakuwa mmetuamini tena kuwa mabalozi wa kuziwakilisha taasisi zetu kwaajili ya kuja kutekeleza mkakati wa pili wa 'haki mtoto'tunaahidi uzoefu ambao tuliupata kupitia utekelezaji wa mkakati wa kwanza tutautumia ile na kuongeza vingine vizuri zaidi".Alisema Beatrece

Aliongeza kuwa watatumia changamoto walizozipata katika mkakati wa kwanza kama fursa ili kuweza kutekeleza mkakati wa pili kwa kiwango cha asilimia 100.


 


Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali ya awamu ya tano itaendelea kulinda kwa nguvu za Mtoto na kwamba haitomvumilia mtu yeyote ambaye atamfanyia ukatili au udhalilishaji mtoto mdogo.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akizindua mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki ya mtoto nchini ya mwaka 2020 hadi 2025 yenye lengo la kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.

Waziri Nchemba pia amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanaupitia mpango huo na kuufanyia maboresho kwa kuutafsiri kwa lugha ya kiswahili ili uweze kuwafikia watu wengi zaidi.

Dk Nchemba amesema uzinduzi wa mpango huo ni nia ya serikali katika kupambana na ukatili kwa Watoto na kuimarisha haki ya mtoto na kutaka mpango huo utafsiriwe kwa lugha adhimu ya Kiswahili ili kila mmoja aweze kuuelewa mpango huo.

" Huu mpango wa kwanza uliotekelezwa kuanzia mwaka 2012 hadi 2017 kuna mazuri yamefanyika lakini tumekuja na mpango huu ambao umeboreshwa zaidi na hii ni nia serikali kuhakikisha inalinda haki ya mtoto,

Nitoe maagizo kwa Katibu Mkuu kuhakikisha mpango huu utafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili sote tunajua hii ni lugha ya ukombozi kwa nchi yetu hivyo ni vema mpango huo utafsiriwe kwa lugha ambayo kila mmoja wetu ataielewa wakati ya kuitekeleza,” Amesema Dkt Nchemba.

Amesema mpango huo umelenga zaidi katika kuongeza uelewa wa haki ya mtoto katika jamii kwa Watoto na wadau mbalimbali, kuimarisha mfumo wa utoaji haki kwa mtoto, kuimarisha mfumo wa ulinzi na usalama wa mtoto, kuboresha sera na sheria, kuimarisha uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango mkakati huu.

Amesema Wizara ya katiba na sheria kwa kushirikiana na jukwaa la haki mtoto itaendelea kuratibu na kufuatilia mwenendo na utekelezaji wa mkakati huu kwa kushirikana na Wizara nyingine zinazotekeleza mpango huo.

Ametoa wito kwa wadau na jamii mbalimbali kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kutekeleza mpango mkakati huo ili Watoto waweze kulindwa na kufurahia upatikanaji wa haki kwa wakati kwa kuwa haki ya mtoto ni  mtambuka.

Waziri Nchemba amezitaka taasisi, mashirika, wadau na jamii kwa ujumla wakati wa kutekeleza mpango huo kuangalia upande wa pili kwa kumuangalia mtoto huyo kwa Maisha yake ya baadaye na badala yake wajue kutofautisha kuvunja haki ya mtoto na maandalizi ya mtoto kwa Maisha yake ya baadaye.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome, amesema katika kulinda haki ya mtoto Wizara imeandaa na kuratibu na kuutekeleza mpango huo wa pili ambapo wamefanya marekebisho mbalimbali ya sheria yote ni katika kulinda hali ya mtoto.

Jitihada nyingine ametaja kuwa ni kuongeza makahama zinazosikiliza haki za Watoto hadi kufikia mahakama 130 na kuwapa mafunzo maafisa 638 wa mahakama waliojengewa uwezo wa kusikiliza mashauri yanayohusu kesi za ukatili dhidi ya Watoto, na mawakili wa serikali na mawakili wa kujitegemea walijengewa uwezo wa kuendesha kesi kama hizo.

Amesema kesi mbalimbali za ukatili dhidi ya Watoto 63,023 zimesikilizwa na kuwapa haki sawa hata watoto wanaotoka katika kaya maskini ambapo walikuwa hawana uwezo wa kuwa na wakili waliweza kusaidiwa ili kuweza kupata haki yao.

Nae Mwakilishi mkazi wa Unicef hapa nchini, Shalini Baragua ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kupambana kuhakikisha haki ya mtoto inalindwa katika ngazi zote mijini na vijijini.

Amesema ulinzi wa mtoto ni suala mtambuka hivyo ni wajibu wa kila mwanajamii kuhakikisha anakuwa mlinzi wa Watoto ili kujenga kizazi imara kwa miaka ijayo na kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.







 

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Geofrey Pinda akijibu maswali bungeni wakati wa mkutano wa 12 Jijini Dodoma, Leo tarehe 5 Februari 2021. (Picha Na Mathias Canal)

Na Matias Canal, Wizara ya Katiba na Sheria-Dodoma

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Geofrey Pinda amewahakikishia watanzania kuwa Serikali haina Sheria Kandamizi hivyo Sheria zote zinazotumika nchini zilitungwa na Bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo halijawahi kutunga Sheria Kandamizi.

Amesema kuwa Serikali kwa kuzingatia mahitaji ya wakati na watu wake, imekuwa ikiwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya Sheria mbalimbali ili kuziboresha Sheria hizo.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe Zainab Katimba aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kurekebisha baadhi ya sheria kandamizi kwa wanawake ili ziendane na wakati, Mhe Pinda amesema kuwa Kutokana na wakati uliopo na mahitaji ya sasa Serikali imeanzisha mchakato wa kuzipitia baadhi ya sheria ili ziweze kufanyiwa marekebisho kuendana na wakati.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa muswada wa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Ndoa utakaowasilishwa Bungeni ili kuiboresha, kwa lengo la kulinda makundi ya wanufaika na Sheria hiyo.

Aidha, Serikali inaendelea na hatua mbalimbali za kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mirathi na Sheria za Kimila. Hatua hizo zikikamilika, Muswada wa mapendekezo ya kuzirekebisha sheria hizo utawasilishwa Bungeni, ili Wabunge wapate nafasi nzuri ya kujadiliana na kuyapitisha marekebisho hayo.  

Mhe Pinda amesem akuwa Wizara ipo katika mabadiliko makubwa ya kuhakikisha kunafanyika maboresho makubwa ya Sheria zetu ikiwemo kuzitafsiri kwa Kiswahili lakini pia kuweka vipengele kwenye sheria hizo vya kutoa hukumu kwa lugha ya Kiswahili jambo ambalo litaleta tija kubwa katika ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu.

Hivyo amewaomba wabunge kuunga mkono juhudi za Serikali katika eneo hilo kwa lengo la kuimarisha utawala wa Sheria na upatikanaji wa haki nchini.

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiangalia picha za waliokuwa Majaji Wakuu wa Tanzania katika banda la Mahakama alipotembeea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiangalia moja ya nyaraaka zinazohusu uendeshaji wa mashauri mahakamani wakati alipotembelea   maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo ya  jinsi  Mahakama inayotembea inavyoendesha shughuli zake alipotembelea  maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo juu ya uendeshaji wa mashauri kwa njia ya mtandao unavyofanywa na Mahakama ya Tanzi wa Mahakama unaofanywa na Mahakama ya Tanzania alipotembelea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo juu ya ujenzi wa Mahakama unaofanywa na Mahakama ya Tanzania katika  maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiangalia moja ya vitabu katika banda la Mahakama ya Haki ya afrika Mashariki alipotembeea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo ya muoneshaji katika banda la Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA) katika maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa waoneshaji katika Banda la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) wanaoshiriki maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiulizia kitu katika moja ya machapisho aliyoyakuta katika banda la Wizara ya Katiba na Sheria alipotembelea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisaini kitabu cha wagenii katika banda la Mahakama alipotembeea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma