Na   Bashir    Yakub.

SHERIA  ZILIZOPITIWA :
1. Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai, Sura ya 20.
2. Sheria  ya Huduma za Mashtaka  kwa Taifa, Na. 27/2008.
3. Kanuni  za  Adhabu, Sura  ya  16.
_______________

Tundu Lissu anasema  anaamua kumshitaki Makonda kwa kosa la kughushi nk. kwa kuwa Serikali imekataa na haioneshi nia ya  kumfikisha mahakamani Makonda.

Kama sababu ni kuwa serikali imekataa kumpeleka Makonda mahakamani  ndio maana  Tundu Lissu na wenzake wanaamua sasa kuchukua hatua basi nao hawatafanikiwa.

Kwa sheria ilivyo hawatafanikiwa mpaka serikali  wanayosema haitaki itake.  Kwa mujibu wa kifungu cha  97 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi  za Jinai kazi ya kufungua na kuendesha mashtaka  yote ya jinai ni kazi ya serikali kupitia  ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).

Hata hivyo  kwa mujibu wa kifungu cha 99(1)  cha sheria hiyohiyo ni kweli bila ubishi kuwa mtu binafsi  au Wakili yeyote binafsi kama alivyo Tundu Lissu naye  anaweza  kufungua na kuendesha mashtaka ya jinai dhidi ya mtu yeyote mkosaji kama ilivyo kwa DPP wa serikali.

Pamoja na hayo kifungu cha  97 cha sheria hiyo ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kinasema kuwa ikiwa mashtaka yamefunguliwa na mtu binafsi au Wakili binafsi kama alivyo Tundu Lissu basi  mwendesha mashtaka wa serikali  akiamua anaweza kuchukua kesi hiyo.
Pia kifungu kinasema zaidi kuwa Wakili huyo binafsi katika kesi hiyo aliyofungua atalazimika  kufuata maelekezo   ya  mwendesha mashtaka  huyo wa serikali wakati wote  wa kesi.
Maana yake ni kuwa ikiwa mwendesha mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kubadili jambo lolote katika kesi aliyofungua basi atalazimika kulibadilisha. Lakini kubwa kuliko yote ikiwa mwendesha mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kufuta kabisa kesi ya Makonda  basi atalazimika kuifuta. Hii ndio maana ya kifungu hicho.
KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...