Serikali imefurahishwa na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Milioni 99,983,700/- kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 6,077,800/- kwa hospitali ya rufani ya Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na changamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini.

Awali, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko huo pamoja na kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa wanachama wake ambao wako kwenye sekta rasmi na sekta isiyokuwa rasmi. Sehemu ya mapato wanarudisha kwenye jamii kupitia sera ya uchangiaji na udhamini,ambapo sekta ya afya ni moja ya sehemu ambayo PPF wanachangia.

Lulu alisema PPF inawajali jamii maana kwenye jamii ndio chimbuko la wanachama wa PPF. Alitoa rai kwa sekta iliyorasmi ambao bado hawajajiunga na Mfuko wowote kujiunga na PPF ili kunufaika na mafao bora kama vile la uzazi ambapo hutolewa kwa mwanachama mwanamke pindi anapojifungua.

Alisema PPF inatoa shilingi 1,000,000 ambayo haikatwi kwenye michango ya mwanachama .Hivyo ni fursa kujiunga na PPF. Naye, Meneja wa Kanda ya Mashariki na kati Michael Christian, alisema pamoja na kuandikisha wanachama kutoka kwenye sekta rasmi vilevile PPF inawaandikisha wanachama waliojiajiri wenyewe kupitia mfumo wake wa 'Wote scheme'.

Alisema Mfuko una fursa mbali mbali kama vile mikopo ya maendeleo,huduma ya afya kupitia NHIF,mikopo ya elimu na mafao ya uzeeni. Aliendelea kwa kusema mfumo huo wa 'Wote scheme' unawaandikisha hata watu waliojiunga na Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii kama mfumo wao wa ziada wa kujiwekea akiba. Katika makabidhiano hayo sehemu ya watu waliojiunga na mfumo wa 'Wote scheme' ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Frak Jacob.

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa kwenye wodi ya wajawazito akiwemo Asia Amani na Gloria Abdalah, waliupongeza Mfuko huo kwa kuwapatia vitanda vya kisasa vya kujifungulia.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufani ya Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mh. Pascal Kihanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba.  Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo.
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...