Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys wameendelea limbwi la ushindi baada ya jana kutoka kifua mbele kwa kuifunga Cameroon katika mchezo wa kirafiki uliofanyika nchini Cameroon.

Timu hizo zitarudiana tena  katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kesho Jumatano, Mei 3, mwaka huu.

Mbali na hilo, Afisa habari wa Shirikisho Alfred Lucas amesema kuwa timu ya Serengeti Boys imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa imepangiwa Libreville.

Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu. Kwa mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na wenyeji Gabon, litakuwa Port Gentil.

Kwa sasa Serengeti Boys wako Cameroon kwa kambi ya wiki moja iliyoanza Aprili 29, mwaka huu ambako tayari imecheza na wenyeji Cameroon mchezo mmoja na kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Yauonde. 

Timu ya Serengeti inahitaji kushinda mechi mbili za mwanzo ili kujihakikishia nafasi ya kwenda kombe dunia  la vijana chini ya miaka 17 litakalofanyika nchini India.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...