Na Karama Kinyunko.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa kesi ya kukutwa na bhangi inayomkabili Msanii maarufu nchini wa filamu, Wema Isaack Sepetu (28) na wenzake wawili umekamilika.

 Wakili wa Serikali, Onolina Moshi aliyaeleza hayo leo  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. 

Mheshimiwa, kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika naomba ahirisho kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH). Amesema Moshi.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo   hadi Juni Mosi,2017 kwa PH.

Wema amewakilishwa mahakamani hapo na Wakili Tundu Lissu.

Mbali na Wema washtakiwa  wengine ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima.Watuhumiwa hao wawili wanatetewa na wakili Peter Kibatala na Hekima Mwesigwa.

 Wema ambaye ni mshindi wa taji ya Urembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 alifikishwa mahakamani hapo na kupandishwa kizimbani baada ya kusota mahabusu katika kituo kikuu cha Polisi (Police Central ) Dar es Salaam kwa muda wa siku Sita.

Awali ilidaiwa kuwa, Februari 4 mwaka huu, huko Kunduchi Ununio, wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili.

Hata hivyo washtakiwa hao wote walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...