Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni(wa pili toka kulia) akiwaongoza kuimba wimbo wa Taifa la Tanzania Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee(hawapo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, (wa kwanza kutoka kushoto) ni Mjumbe wa Sekretarieti ya SADC, Bw. Maemo Machete. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni kufungua rasmi mkutano huo wa siku moja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee uliofanyika leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao hicho kama inavyoonekana katika picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...