NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

TAASISI ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya Ziwa imetoa msaada wa vyakula anuwai vya futari na daku kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa na mahabusu 400 wa Gereza Kuu la Butimba Mwanza.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi futari hiyo kwenye gereza hilo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Kanda ya Ziwa Alhaji Sibtain Meghjee alisema msaada huo wa vyakula utawapa fursa ya kufunga na kuwajenga kiimani na hatimaye kuwa raia wema watakapomaliza kutumikia adhabu zao gerezani.

Mbali na futari hiyo yenye thamani ya shilingi 3.5 milioni ambayo ni mchele kilo 500, sukari kilo 200, unga wa sembe kilo 400, mafuta ya kula lita 60 na kuni tani tatu pamoja na vitabu mbalimbali vya dini ya Kiislamu kwa ajili ya kujifunza masomo ya dini hiyo muda wote watakaokuwa gerezani.

Alhaji Sibtain aliushukuru uongozi wa Gereza la Butimba akisema wataendelea kushirikiana na watakuwa tayari kupeleka masheikh wa kwenda kutoa mafundisho ya dini kwa wafungwa na mahabusu kwa gharama zao ili kuwajenga na watakaporudi uraiani wasirejee kufanya makosa.

Kwa Upande wake Sheikh wa Bilal Muslim wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Hashim Ramadhani alisema msaada huo utawapa fursa zaidi ya kuwafanya wawe karibu na Mwenyezi Mungu.

Kiongozi wa wafungwa na mahabusu hao Yasin Said akitoa shukurani zake huku akinukuu aya na maandiko mbalimbali alisema wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani aliye huru aanapaswa amkumbuke aliye kifungoni kwa kumtaja kwa wakubwa ili apewe taklififu (unafuu) bila kusahaulika.

“Pamoja na Allah (S W T) pia kuna riziki za wafungwa ambazo hutolewa bila kutarajia kupata chochote bali radhi ya Allah.Waliokuchukizeni na kuwakwaza msilipize kisasi kwa jeuri na chuki, bali saidianeni nao katika kufunga, kuswali, kusoma, wema na kumcha Mungu na si katika dhambi na uadui,” alisema Said.

Aliongeza kuwa msaada huo utawasaidia kuwafanya wawe watu wema zaidi na kufanya ibada za kufunga na kuswali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...