Jirani yako au
mtu mwingine yeyote
amejenga na kuziba
njia. Njia yoyote iwe kubwa
kama barabara ama
ndogo ambayo hata
gari haiwezi kupita. Iwe
tu kama ya pikipiki
au baiskeli au hata ya
miguu tu. Yote
haya hayajalishi na hizi
zote ni njia kwa
mujibu wa sheria.
1.HAKI YA
NJIA KISHERIA .
Kifungu cha 151
cha sheria namba
4 sheria ya
ardhi ya mwaka
1999 kinaeleza haki hii. Kinaitambua haki
hii kwa kusema
kuwa haki ya
njia ipo kwa
njia zile ambazo
ni kwa ajili ya
matumizi ya umma.
Umma hapa humaanisha
watu wote lakini
pia wakazi wa
eneo fulani wanaotumia
njia hiyo kwa
ajili ya shughuli
zao mbalimbali.
Kifungu kimepanua
matumizi ya njia
ya umma kwa
kumaanisha hata njia
zilizotengwa kwa ajili ya
makampuni binafsi.
Kwa mfano
kuna sehemu ukipita
utaona njia au sehemu
ya lami ya
barabara imekatwa maalum kwa
ajli ya kuruhusu watu
au magari ya kampuni
fulani kupata sehemu
ya kuingilia.
Lakini pia zipo
njia zimetengwa kwa
ajili ya shughuli
za serikali. Haraka utaona kuwa haki
ya njia haijagusa tu kule
mitaani wanakoishi watu
tu bali hata
sehemu za makampuni
binafsi nk.
2. KUZIBA
NJIA YA UMMA.
Kuziba njia ya
umma ni kosa
kwa mujibu wa
kifungu cha 177( 4 )
cha sheria ya
ardhi. Wako watu wakorofi
huko mitaani huziba
njia kwa makusudi.
Yawezekana kabisa mtu akiwa
anajua kabisa eneo fulani ni
njia na watu
hupita hapo lakini
kwa makusudi au bila kujali
akajenga ukuta au akaweka
uzio wa
sinyenge au akapanda
mti pale au
akaweka kifusi au kwa
namna nyingine yoyote.
Na wengine huambiwa
na watu lakini
wasisikie kwasababu ya
pesa, au urafiki
na viongozi wa
serikali au cheo
au rushwa au
vinginevyo. Basi yatupasa
kujua kuwa watu hawa
huwa wakitenda makosa
na si wakunyamazia.
Njia kuzibwa si lazima
iwe imezibwa yote. Hata kuibana na kuitoa katika
uhalisia wake katika
kiwango chochote nako
ni kuziba njia.
Njia yafaa iachwe
vilevile ilivyo.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...