Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amewataka wananchi wanaoishi katika mikoa itakayopitiwa na miundombinu ya bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

Dkt. Pallangyo aliyasema hayo mapema jana jijini Dar es Salaam kupitia kipindi maalum cha 360 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds wakati akielezea maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu.

Alisema kuwa wananchi katika maeneo husika wanatakiwa kujiandaa kwa ajira wakati wa maandalizi na utekelezaji wa mradi, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za vyakula, usafiri na ufundi.

“Fursa zitakazokuwepo ni nyingi mno, vijana waliomaliza Vyuo vya Ufundi wataweza kufanya kazi za uchomeleaji wa vyuma, madereva wenye leseni kupata kazi, wakina mama lishe kuuza vyakula, wakulima kuuza mazao kwa walaji watakaoongezeka kutokana na uwepo wa mradi huo, alisema Dkt. Pallangyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari na mwongozaji wa kipindi cha 360 cha Clouds TV, Hassan Ngoma katika mahojiano maalum kuhusu uzinduzi wa mradi wa wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu yaliyofanyika mapema Julai 31, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa habari na mwongozaji wa kipindi cha 360 cha Clouds TV, Hassan Ngoma akiuliza swali kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) kwenye mahojiano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...