Na Rajabu Mkasaba, IKULU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya kimaendeleo baada ya kuundwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar kumeweza kuongeza mapato na kuahidi kuimarika zaidi hali hiyo ndani ya kipindi chake cha uongozi. 
Dk. Shein aliyasema hayo leo, alipokutana na uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege katika vikao vinavyoendelea Ikulu mjini Zanzibar. 
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuipongeza Mamlaka hiyo kwa kufanya mabadiliko makubwa katika viwanja vya ndege vya Zanzibar hatua ambayo imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato katika viwanja hivyo. 
Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa licha ya baadhi ya changamoto zilizopo lakini Mamlaka imeweza kupata mafanikio makubwa na hivi leo viwanja vya ndege Unguja na Pemba viweza kuimarika na kuleta tija kwa kuongeza mapato. 
Akizungumza suala zima la fidia kwa wananchi waliojenga pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar Dk. Shein alisema kuwa ni vyema likatafutiwa ufumbuzi kwa kuwatafuta wahusika na kuwasikiliza madai yao ili hatua za malipo ziendele kuchukuliwa. 
Akizungumza na uongozi wa Wizara hiyo kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba pamoja na Uongozi wa Shirika hilo, Dk. Shein alisisitiza haja ya Shirika hilo kuzitambua na kuziorodhesha ili kujua idadi ya nyumba zao zote za Unguja na Pemba pamoja na zile za Wakala hatua ambayo pia, itasaidia kuepusha udanganyifu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akionesha Ramani ya Ujenzi wa Mji wa kisasa utakaojengwa  sambamba na ufukiaji wa Bahari ya  Eneo la pwani ya Gulioni  katika kikao cha siku moja kilichojumuisha  Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Wajumbe  wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba na Uongozi wa Shirika la Nyumba  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akionesha Ramani ya Ujenzi wa Mji wa kisasa utakaojengwa  sambamba na ufukiaji wa Bahari ya  Eneo la pwani ya Gulioni  katika kikao cha siku moja kilichojumuisha  Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Wajumbe  wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba na Uongozi wa Shirika la Nyumba  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja 
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofanya kikao cha siku moja pamoja na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. Kwa Taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...