Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KUELEKEA mtanange wa kumaliza ubishi baina ya mahasimu wawili Simb ana Yanga huku kila upande ukijinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kesho kuanzia majira ya saa 11 jioni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Ni mechi ya watani wa jadi inayozungumzwa sana midomoni mwa watu, kila mmoja akijinasibu kumfunga mwenzake kwa idadi kubwa ya magoli na na kuinyakua Ngao ya Jamii.

Simba ikiwa imefanya usajili mkubwa sana na wagharama, wakiwajumuisha nyota wanne kutoka Azam Fc John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Erasto Nyoni pamoja na Kiungo Mnyarwanda kutoka Yanga aliyekipiga kwa misimu kadhaa Haruna Niyonzima.

Mbali na hao, wamemsajili golikipa wa Timu ya Taifa akitokea Mtibwa Sugar Said Dunda na Emanuel Mseja kutoka Mbao Fc, beki wa kulia Shomary Ally, beki wa kati kutoka Toto Africa Yusuf Mlipili, Salim Mbonde kutoka Mtibwa na Mshambuliaji Emanuel Okwi kutoka Sc Villa ya Nchini Uganda. Nicolaus Gyan kutoka Nchini Ghana na beki wa kushoto kutoka Mbao Jamal Mwambeleko 

Kwa upande wa Yanga, wameweza kufanya usajili kwa kuwasajili Ibrahim Ajib kutoka Simba, Raphael Daud kutoka Mbeya City, Pius Buswita kutoka Mbao Fc, Gadiel Michael kutoka Azam, Papii Kabamba Tshishimbi wa Mbabane Swallows na wameweza kuwapanisha vijana wao kutoka timu B Said Musa, Maka Edward ili kuja kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wachezaji walioachwa pamoja na wale waliosajiliwa na timu zingine.


Yanga walifanikiwa kuwabakisha wachezaji muhimu kama Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe waliokuwa wamemaliza mikataba ya kuitumikia klabu hiyo ya Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...