Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
WAFANYABIASHARA
wawili wakazi wa Kimara jijini Dar es Salaam, Jumbo Cheto(39) na
Anna Kilawe (43) leo wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mafuta ya mawese
na sabuni zenye thamani ya milioni 60.
Hati
ya mashtaka imesomwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa
Kishenyi ambae amedai siku na mahali pasipojulikana, wote wawili
walikula njama ya wizi iloyokuwa safarini.
Imedaiwa,
kati ya Mei 19 na 23, mwaka huu, huko kinondoni washtakiwa hao waliiba
magaloni 1056 za mafuta ya mawese ya Lita 20, madumu mengine ya Lita
200 na sabuni 1319 ambapo vitu vyote vina thamani shilingi milioni 60.
Washtakiwa wamekana mashtaka hayo na kwai hiyo itatajwa tena Agosti 30, mwaka huu.
Mfanyabiashara, Jumbo Cheto(39) mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mafuta ya mawese na sabuni zenye thamani ya milioni 60.
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mafuta ya mawese na sabuni zenye thamani ya milioni 60.
Mfanyabiashara, Anna Kilawe (43) mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam (Mwenye nguo ya Pink) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mafuta ya mawese na sabuni zenye
thamani ya milioni 60.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...