Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua zoezi la Ulipaji wa fidia kwa Wakazi wanaopitiwa na Mradi wa uboreshaji wa Barabara kwa maeneo yasiyopangwa DMDP,ambao wataanza kulipwa Fedha zao kuanzia kesho sambamba na kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Barabara.
Mradi huo utahusisha  uboreshaji wa Barabara,Mabonde ya Mito, Ujenzi wa Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala ambapo unagharimu kiasi cha Shilingi Billion 230.
Miongoni mwa Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia Morocco hotel hadi Sinza Kijiweni Km 5, Barabara ya Tandale Kisiwani kuelekea Mwananyamala na Barabara za Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200, Kilungule na MMK.
Makonda amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.Amewataka wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kutafuta makazi bora sehemu nzuri zaidi na pia kufanyia shughuli zingine za kimaendeleo zitakazo waingizia kipato.
Aidha Makonda amesema kuwa Kata za Tandale, Mburahati na Mwananyamala zitaingizwa kwenye idadi ya Kata 14 zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za kisasa maana ya kuwa na Lami,Taa na Mitaro ya Maji.Hata hivyo amesema Mto Ng’ombe pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa Km 7.5 ili kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.
Makonda amempongeza Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta na Manispaa hiyo na kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile anachostahili bila usumbufu.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipata maelezo mafupi kutoka kwa baadhi ya Wananchi kuhusu maeneo ambayo miundombinu yake imekuwa kero kwa wananchi,ikiwemo makaravati yaliyoziba na mitaro 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi akizungumza na baadhi ya wananchi walioko kwenye kituo cha daladala cha Simu 2000 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi wakikagua miondombnu mingine ikiwemo madaraja na makaravati yaliyoziba,ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi wakikagua barabara ya Makumbusho mapema leo jijini Dar.Picha na Emmnanuel Masaka-Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...